Pages

Thursday, October 4, 2012

THOMAS ULIMWENGA APIGA GOLI MBILI MAZEMBE IKIUWA 5




MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya nchini DR Congo, Thomas Ulimwengu, jana aliibuka shujaa baada ya kuisaidia klabu yake kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo.
Katika mchezo TP Mazembe ilichomoza na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya  A.S Vutuka ambapo mshambuliaji huyo raia wa Tanzania alizifumania nyavu mara mbili katika ushindi huo mkubwa.
Mabao mengine ya Mazembe yalifungwa na Stopila Sunzu ambaye ni  mdogo wa mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu, aliyefunga bao moja huku mengine yakifungwa na Eric na Ilongo.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo. Ulimwengu alisema anamshukuru Mungu kwa kumsaidia kuonyesha uwezo mkubwa kwa kufunga mabao hayo ambayo yaliisaidia timu yake kujiimarisha katika ligi hiyo.
“Namshukuru Mungu kwa kunisaidia kufanya vizuri katika mchezo wa leo, ushindi ambao naimani utaisaidia klabu yangu,” alisema Ulimwengu.

No comments:

Post a Comment