Pages

Monday, October 29, 2012

YANGA YAREJEA SALAMA DAR WACHEZAJI WOTE WAPO FITI WAENDELEA NA MAZOEZI LOYOLAI





Mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (KAGAME),timu ya Yanga imeendelea na mazoezi leo asubuhi katika Uwanja wa shule ya sekeondari Loyola tayari kwa ajli ya kuikabili timu ya Mgambo JKT siku ya jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha wachezaji 20 na Benchi la Ufundi 7 kilirejea jana jioni kutokea jijini Arusha ambapo katika mchezo wake dhidi ya timu ya JKT Oljoro ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, shukrani kwa bao lililofungwa na mlinzi wa kati Mbuyu Twite dakika ya 53.
Wachezaji wote wamefanya mazoezi asubuhi ya leo, kitu ambacho kocha Ernie amefurahia kutokua na majeruhi hivyo anamini kikosi chake kiko tayari kuivaa timu ya Mgambo JKTkatika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Kwa matokeo hayo, Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa pointi 20, ikiwa nyuma ya watani wa jadi Simba wenye pointi 22 huku waoka mikate timu ya Azam FC ikiwa katika nafasi ya nne, baada ya timu ya Coastal kushinda jana na kufikisha pointi 19.
Kocha mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahishwa na mabadiliko ya kiuchezaji ya kikosi chake,kwani wachezaji wake kwa sasa wanaonyesha kumuelewa anavyotaka wacheze,hivyo anaamini mabadiliko mengi yataonekanakadri siku zinavyokwenda.
Brandts ameongeza kwamba anapenda wachezaji wake wacheze pasi za haraka haraka huku wakipanga mipango ya mashambulizi, na kwa sasa anaona wachezaji wanaanza kumuelewa hali inayopelekea timu kuibuka na ushindi wa 4 mfululizo.
Katika michezo itakayochezwa siku ya jumatano, endapo Yanga itashinda na Simba ikatoka sare basi Yanga itakamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
Young Africans imebakisha michezo michezo 3 kabla ya kumalizika kwa duru la mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara

No comments:

Post a Comment