Pages

Sunday, November 25, 2012

CHECK PICHA ZA MATUKIO JAMAA AMSHIKA DEMU WA BAUNSA ANAKULA KICHAPO CHALI HHAHA! MAKUBWA HAYA! MKE WA MTU SUMU



KIJANA mmoja ambaye jina lake halikunaswa mara moja juzikati alikumbwa na gharika kama siyo ajali ya kukandamizwa konde mpaka kuzimika, kisa ni kikiwa ni kumshika sehemu nyeti mke wa ‘baunsa’.

Pita pita ya paparazzi wetu zilinasa tukio hilo  ndani ya ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam, ambako alimkuta kijana huyo akipepewa ili arudishe pumzi.
Ukurasa wa maelezo ya mashuhuda ulisomeka kwamba, kabla ya kipigo kijana huyo alikuwa akitandika ‘maji makali’ na mwanamke mmoja aliyemtambulisha kama ‘maiwaifu’ wake.

Inaelezwa, safisha koo ilipokolea, huduma ya upakuaji maji taka ilihitajika mwilini, ndipo jamaa huyo alipomuaga mkewe kwamba anakwenda maliwatoni kujihifadhi.

Dondoo zinaweka wazi kwamba, hatua chache baada ya kunyanyuka kwenye kiti, jamaa alikutana na msichana mdogo mweupe, ambaye alijikuta amemshika kiunoni, kwa tamaa au vinginevyo hilo halikuelezwa
.
Kama msemo wa wahenga usemavyo, mke wa mtu sumu, baunsa mwenye ‘kipoozeo hicho’ anadaiwa kuona mchezo huo, ambapo alifyatua kombora la ngumi iliyompata kijana huyo shavuni na kuzimia.

Makelele ya ‘kaua, kaua’ yalipotawala ukumbini, baunsa alitimua mbio na kumuacha mke wa kijana aliyezimia akilia na kuomba msaada wa wasamaria, waliojitokeza na kumkimbiza majeruhi hospitali

No comments:

Post a Comment