MADIWANI
wa Chama cha Demokrasia na maendeleo(Chadema) wilayani Arusha
waliogoma kumtambua Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo sasa wanadaiwa
kuanza kumtambua kwa kupitia ‘mlango wa nyuma’.
Tangu ufanyike uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha, kumeibuka mvutano wa kisiasa uliosababisha Chadema wawatangazie wananchi kutomtambua Meya huyo.
Tangu ufanyike uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha, kumeibuka mvutano wa kisiasa uliosababisha Chadema wawatangazie wananchi kutomtambua Meya huyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Omari Mkombole akizungumzia matumizi ya
fedha zilizotumika katika uzinduzi wa Jiji hilo hivi karibuni alisema
kwamba
madiwani wa vyama vyote walishiriki vikao muhimu vya kufanikisha sherehe hizo.
Lakini
itakumbukwa ya kwamba msimamo wa madiwani wa Chadema kutomtambua meya
huyo ulikuwa ni kutoshiriki vikao vyote vya jiji hilo kama ishara ya
kusimamia msimamo wao.
Tayari
baadhi ya makada wa Chadema jijini hapa wametoa msimamo wao kwa nyakati
tofauti wakati wakihojiwa kuhusiana na hali hiyo ambapo baadhi ya
wamelaani kitendo hicho huku wakienda mbali zaidi na kusema kwamba
kitendo hicho ni unafiki mkubwa.
“Taarifa
zilizonukuliwa nje kama ni siri zilikuwa ni makisio ya bajeti ambayo
baada ya kupitiwa ilibadilishwa na kupata bajeti halisi ya sherehe, hili
si siri nyaraka madiwani waliohudhuria wanazo vikao vyote hivi
vilifanyika kwa ushirikiano wa madiwani wa Tlp, Chadema wasiokuwa na
mivutano na chama chao na CCM chini ya Meya wa Jiji la Arusha,” alisema
Mkombole
Mkombole,
akichanganua fedha hizo alisema, zilikuwa ni Sh. 123,689,550 milioni
ambapo Mamlaka ya Maji Safi na Taka Arusha (AUWSA) walichangia Sh.
18,156,500 fedha zilizokarabati mnara wa Azimio la Arusha.
Alisema
mdau mwingine Kampuni ya Jiangxi- Geo –Engeneering (Group) Corporation
inayojenga barabara za Jiji la Arusha ilichangia Sh, 12 milioni ,
kampuni ya China Railway Seventh Group Co Ltd ilichangia Sh , 4 milioni
na kufanya jumla ya Sh Milioni 35 kuchangwa na wadau.
“Halmashauri
ya Jiji la Arusha yenyewe imetumia Sh,89,533,050 milioni kugharamia
sherehe hizo kwa shughuli mbalimbali zilizobakia mbali na kuwalipa
wasanii mbalimbali walioalikwa, fedha hizo pia zilitumika kugharamia
chakula cha Rais Kikwete, msafara wake na wageni waalikwa Hoteli ya Mt.
Meru,” alifafanua kaimu mkurugenzi huyo
Akifafanua
kuhusu chakula hicho Mkombole alibainisha kwamba kamati iliyokuwa
inasimamia chakula cha Rais Kikwete ilikuwa ikiongozwa na Efatha Nanyaro
ambaye ni diwani wa Kata ya Levolosi (Chadema) akishirikiana na Paul
Mathysen Diwani wa Moshono kupitia CCM.
Alisema ushiriki wa viongozi hao ambao ni wawakilishi wa wananchi jijini Arusha ulionyesha kwamba suala hilo lilifanyika kwa ridhaa ya Baraza la Madiwani kwa niaba ya wananchi.
Alipotafutwa
mwenyekiti wa madiwani wa Chadema jijini hapa,Isaya Doita ambaye ni
diwani wa kata ya Ngarenaro alikiri wao kushiriki hatua zote katika
maandalizi ya uzinduzi wa jiji hilo na kudai kuwa walipokea posho kwa
kuwa ni haki yao na wana njia mbalimbali za kutomtambua meya wa jiji la
Arusha.
No comments:
Post a Comment