Pages

Monday, November 19, 2012

Mh. Lowassa aongoza Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Babati Mkoani Manyara leo



Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
 akihutubia 
waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) 
usharika wa
 Babati wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa hilo
 Usharika wa Babati,Mkoani Manyara leo.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni 
(wa tatu kulia) 
akizungumza wakati wa Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Kanisa la
 Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,Mkoani
 Manyara leo.Wengine pichani toka Kushoto ni Waziri Mkuu 
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa 
(ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Harambee hiyo),
Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri na Kulia ni
 Diwani wa kata ya 
Endamilay (CCM) Gesso Bajuta.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
 Lowassa akimpongeza Mbunge wa Viti maalum Mkoani
 Manyara (Chadema),Mh. Pauline Gekul mara baada ya
 kuchangia kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la 
Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,
Mkoani Manyara leo.Kulia ni Mbunge wa Jimbo la 
Babati Vijijini,Mhe. Jitu Vrajlal Soni.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa 
akiendelea kupokea michango mbali mbali kwenye Harambee ya
 Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika
 wa Babati,Mkoani Manyara leo. 
Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wakiwa kwenye Harambee hiyo ya Ujenzi wa
 Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Babati,
Mkoani Manyara leo.

No comments:

Post a Comment