Pages

Monday, November 5, 2012

Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Mkoani Kilimanjaro,Charles Ndagula,amenusurika kuuawa baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wafanyabiashara wa magendo ya sukari kumgonga na gari na kuumiza sehemu mbalimbali za mwili.



Mwandishi wa habari Charles Ndagula akiwa amelazwa hospitali ya St Joseph iliyoko mjini moshi kwa ajili ya matatibabu baad ya kugongwa kwa makusudi na wafanyabiashara wanaosafirisha magendo ya sukari kwenda Kenya.Picha na Habari na Rodrick Mushi
---- Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima Mkoani Kilimanjaro,Charles Ndagula,amenusurika kuuawa baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wafanyabiashara wa magendo ya sukari kumgonga na gari na kuumiza sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumza kwa shida akiwa amelazwa hospitali ya St Joseph iliyopo Mjini hapa Ndagula alisema kuwa aligongwa na gari dogo aina ya Toyota Rava4 yenye namba T 265 AUE.

Ndagula alisema kugongwa kwake kumekuja baada ya kupata taarifa kwa mtoa taarifa ya kuwepo magari zaidi ya 12 ambayo yalikuwa yamepakia sukari, tayari kwa ajili ya kwenda Kenya kwa kupitia njia za panya Wilayani Rombo.

Alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo akiwa na mwandishi mwenzake wa Mwananchi,Daniel Mjema,walianza kufuatilia magari hayo kupitia njia ya Holili kuelekea Rombo ikiwa ni majira ya saa 6:00 usiku.

Walipopita eneo la Holili kuelekea Rombo eneo ambalo linachimbwa udongo wa ‘pozolana’ ambao unatumika kutengenezea sementi ndipo walipokutana na magari mawili yakiwa na sukari aina ya fuso yenye namba T 288BHF na lingine likiwa na namba T280 BUZ.

Alisema baada ya kuona magari hayo yakiwa na sukari walimtaarifu kamanda wa Polisi Robert Boaz kumueleza kilichokuwa kinaendelea.

Wakati wakiwa bado katika eneo la tukio wakiendelea na kazi,ambapo zaidi ya magari nane yakiwa na sukari yalikuwa yamekwishapita, ndipo ilifika gari ndo,aina ya Toyota RAV4 yenye namba T265 AUE na kupaki mbele ya alipokuwa amesimama Ndagula.

Alisema kuwa akiendelea kuandika namba za magari yaliyokuwa yanapita,ikiwemo pamoja na gari ndogo ambalo linasadikiwa kuwa mmoja wa wafanyabishara mwenye mzigo huo wa magendo.

“Wakati nikiwa nimesimama mbele ya gari dogo,ndipo mtu mmoja alitoka kwneye magari mawili yalikuwa yamepaki na kuingia kwenye gari dogo na kunifuata nilipokuwa na kunigonga na kuanguka”Alisema Ndagula.

Hata hivyo alisema kuwa kilichosaidia ni kuliona gari dogo wakati likimfuata kwa makusudi kwa lengo la kumgonga na kulikwepa lakini likamuumiza sehemu mbalimbali za mwili.Hata hivyo jitihada za kumtafuta kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro,Robert Boaz kudhitisha tukio hilo zimeshindikana baada ya kupiga simu yake ya mkononi bila kupatikana.

Swali la kujiuliza ni kwamba Polisi wetu  na viongozi wa usalama wanafanya kazi gani kama watu wachache kwa maslahi yao binafsi wanaamua kuvunja sheria zilizowekwa na hili siyo kwamba wamekuwa hawafahamu la hasha biashara ya megendo ipo na inaendelea kufanyika kila kukicha.

No comments:

Post a Comment