Rais Barack Obama akiwasili Burma.
Rais Barack Obama wa Marekani leo anafanya ziara ya kihistoria nchini Myanmar inayolenga kuhimiza mageuzi ya kisiasa.
Rais
Obama atakuwa rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga Myanmar huku nchi
hiyo ikichipuka kutoka miongo kadhaa ya utawala wa kijeshi na kutengwa
na jamii ya kimataifa.
Anatarajiwa
kumpongeza rais wa taifa hilo Thein Sein, kwa kuimaliza enzi ya utawala
wa kijeshi na kumruhusu kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi, kuingia
katika ulingo wa siasa.
Rais Obama atakutana pia na Aung San Suu Kyi nyumbani kwake alikotumikia kifungo cha nyumbani kwa miaka kadhaa.
Baadaye leo Obama atakwenda Cambodia kuhudhuria mkutano wa kilele wa mataifa ya Asia Mashariki.
Hata hivyo Obama atamshinikiza rais Sein kuongeza kasi kuelekea demokrasia halisi.
No comments:
Post a Comment