Pages

Tuesday, November 13, 2012

Wanafunzi Dar na foleni ya mabegi wakupanda treni

Baadhi ya wanafunzi wanaosafiri kwa treni kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea Ubungo wakiwa wamepanga mabegi yao kwenye mstari huku wao wakiwa wamepumzika pembeni wakisubiri usafiri huo. Kwa utaratibu wa kawaida wa usafiri huo abiria hutakiwa kupanga foleni ili inapowasili kila abiria aingie kadri ya ulivyowahi kwenye foleni hiyo. 

BAADHI ya Wanafunzi jijini Dar es Salaam ambao hutumia treni ya abiria inayofanya safari zake Ubungo na Katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni) wamebudi staili mpya ya kuepuka kupanga mstari mrefu huku wakisimama muda mrefu kusubiri usafiri huo.

 Wanafunzio hao wanapofika mapema kituoni hupanga mabegi yao kwa mstari na wao kupumzika pembeni hadi treni inapofika ndipo huinuka katika maeneo mbalimbali waliokaa na kuingia kwenye mstari kwa kufuata begi la mtu. Begi moja kwenye mstari humwakilisha mwanafunzi mmoja. Thehabari imeshuhudia utaratibu huu waliobuni wanafunzi kuepuka wao kusimama muda mrefu wakiisubiri treni kuwasili kituoni. 

Kikawaida abiria wanaosafiri kwa treni hiyo wakiwemo wanafunzi husimama kwa foleni kwa muda mrefu wakisubiri usafiri huo, huku kukiwa hakuna viti vya kutosha kupumzikia wasafiri wanaposubiri usafiri huo.

No comments:

Post a Comment