Pages

Thursday, November 1, 2012

WATU NA PESA ZAO!! SHABIKI WA MOVIE ZA JAMES BOND KUFUNGA HARUSI KWENYE HIZI NDEGE ZILIZOTUMIKA KTK HIZO MOVIE.



Milionea Abdul Hasan mwenye umri wa miaka 23 amefanya uamuzi wa kulipia ndege tatu zilizowahi kutumika kwenye utengenezaji wa movie za James Bond ambapo ndege gizo hizo zitatumika kwenye harusi yake itakayofungwa angani, ametaka iwe hivyo kwa sababu anapenda sana movie za James Bond yeye na mkewe mtarajiwa.
Pamoja na hayo Abdul amesema kwenye hiyo harusi ambayo anataka iwe ya kijames Bond amempata mtu anaefanana na Daniel Craig ambae pia ni staa wa movie za James Bond, harusi itafungwa angani kwenye hiyo ndege hapo juu na itahudhuriwa na watu 200 tu.
Abdul na mpenzi wake wakiwa na jamaa anaefanana na mmoja kati ya mastaa waliowahi kuigiza kwenye movie za James Bond.
Wametumia miezi 10 kuandaa hii harusi.
Abdul na mke wake watatumia helikopta iliyotumika kwenye movie ya James Bond ya GoldenEye mwaka 1995 kwenda honey moon.

No comments:

Post a Comment