Sonali
Mukherjee akiwa kwenye kipindi maarufu cha ‘Who want to be a
Millionaire’ kinachorushwa kwenye televisheni za India sambamba na Lara
Dutta na Muongozaji wa Kipindi hicho Amitabh Bachchan al maarufu kama
Big
Mwathirika
katika tukio la kutisha la kumwagiwa tindikali usoni ameshinda Bingo
katika kipindi maarufu nchini India cha Televisheni.
Sonali
Mukherjee aliharibiwa sura yake baada ya kushambuliwa kwa kumwagiwa
tindikali usoni akiwa binti wa miaka 17 huku familia yake ikibaki tupu
kwa kugharamia matibabu yake.
Sonali Mukherjee anavyoonekana hivi sasa baada ya kumwagiwa tindikali.
Sonali
ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 27 anayetoka katika jiji la New Delhi
sasa ataweza kulipia awamu nyingine ya upasuaji baada ya kushinda
zawadi ya juu kabisa ya kipindi ‘Who Wants to be a Millionaire’
kinachoendeshwa nchini humo.
Mwadada
huyo aliyeshambuliwa na mtu aliyekuwa na rafiki zake, ameshinda Rupia
Laki 25 sawa na takriban paundi 30,000 wakati alipoonekana katika hicho
cha televisheni akiwa muigizaji maarufu wa India aliyewahi kuwa ‘Miss
Universe’ Lara Dutta.
Sonali Mukherjee kabla hajamwagiwa tindikali.
Muongozaji
wa kipindi hicho cha luninga Amitabh Bachchan maarufu kwa Jina la Big B
nchini India amempongeza Sonali kwa kujitokeza katika kipindi hicho.
Sonali Mukherjee akiwa kwenye msongo wa mawazo.
No comments:
Post a Comment