JESHI la Polisi limetoa siku saba kwa baadhi ya askari
kuzisalimisha fedha zipatazo sh milioni 150 wanazodaiwa kuiba, ambazo
zilizoporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston jijini Dar es
Salaam juzi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum,
Suleiman Kova, alisema kutokana na tuhuma hizo jeshi hilo limeunda Jopo
la wapelelezi ili kujua ukweli wa madai hayo.
Alisema
Jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi
Kanda Maalum, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi
inavyowezekana, ukweli upatikane ili wananchi wajulishwe matokeo.
Kamanda
Kova alisema jeshi hilo lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake
inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili
ya kazi yake.
Alisema
tukio hilo halikubaliki hivyo kila aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni
lazima ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane
haraka kuondoa shaka shaka kwa wanachi.
Kova
alimtahadharisha Msangi kuwa, endapo atashindwa kutoa majibu ya
kuridhisha basi atambue hata yeye itabidi awajibike ambapo alisema vitu
kama hivi vikiachwa viendelee vinaliletea jeshi hilo sifa mbaya na
kupoteza imani kwa wananchi.
“Pamoja
na kumkabidhi kazi hiyo Msangi lakini hata mimi sitakaa kimya bali
nitalifuatilia kwa karibu ili mradi tuwapatie wananchi ukweli”alisema
Kova.
Alibainisha
kuwa hawezi kupinga kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo
viovu bali suala hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo, ni vema
wananchi wenye ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana
fedha hizo.
Aidha,
Kova alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi zake kwa nidhamu, uaminifu
na ueledi kwani endapo ofisa au askari atakiuka maadili ya kazi yake,
basi hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi yake bila kuchelewa.
Hata
hivyo, katika hali ya kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe
bila kushirikisha wadau wengine kwa madai kuwa, eti lifanya kazi kwa
kutii sheria zote bila kwenda kinyume.
No comments:
Post a Comment