watoto
wanaendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wakichora katuni wakati walipotembelewa
na mchoraji katuni, Nathan Mpangala kupitia program yake ya Wafanye
Watabasamu ambapo pia aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni, ndugu
na marafiki wa Wafanye Watabasamu, jana.
Mchorajiwa
katuni Nathan Mpangala akiangalia jinsi watoto wanavyochora katuni
wakati alipowatembelea katika hospitali ya Muhimbili jana
Mtoto
Aisha akionesha ufundi wake wa kuchora wakati mchoraji katuni Nathan
Mpangala na rafiki zake walipowatembelea na kuchora nao katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, jana.
Mtayarishaji
na mtangazaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa Chanel 10,
Bi. Hoyc Temu, akipata maelekezo ya kitaalam ya jinsi ya kuchora toka
kwa mmoja wa watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika
hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, jana. Matukio ya
ziara hiyo yatarushwa na kipindi hiko hivi karibuni.
Mchoraji
katuni, Nathan Mpangala kwa kushirikiana wachoraji wenzake, familia,
ndugu na marafiki atatembelea watoto wanaosumbuliwa na saratani katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiwa ni muendelezo wa kazi za kijamii
kufuatia Tuzo ya Mchoraji Bora wa katuni 2011 aliyopewa na Baraza la
Habari Tanzania (MCT) na miaka sita ya Mtukwao maarufu kwa jina la
Kibonzo kinachorushwa ITV.
Ziara hiyo ina malengo yafuatayo:
Kuwapatia wagonjwa zawadi mbalimbali.
- Kuchora nao pamoja. Kwa kuwa katuni zina zinachekesha, zitawasaidia watoto hao kupunguza uwoga wa mazingira ya hospitali, zitawasahaulisha maumivu na kuwafanya kuwa bize na kufurahia siku yako.
Katika
ziara hiyo Mpangala aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni na
marafiki wa Programu ya Wafanye Watabasamu na kuwapa zawadi watoto
zawadi mbali kisha wakapata nafasi ya kuchora nao michoro ya kawaidha na
ile ihusuyo maisha yao ya kila siku hospitalini hapo.
Kwa
niaba ya watoto, Mpangala anaishukuru familia yake, ndugu na marafiki
wa Programu ya Wafanye Watabasabu kwa zawadi mbalimbali walizochangia
ambazo zimefanya ziara hiyo kuwa ya mafanikio.
Pia
anashukuru wachoraji wote waliojitokeza na kuungana naye Muhimbili
kwani uwepo wao ulirahisisha usimamiaji wa zoezi la uchorajikwani kila
mtoto alisikilizwa pale alipohitaji maelekezo hivyo kufanya watoto.
No comments:
Post a Comment