Pages

Monday, December 24, 2012

MISAFARA YA WACHAGA NA WAPARE WAKIELEKEA ‘KUHIJI’ MAKWAO TAZAMA PICHA



Wakati ikiwa zikiwa zimesalia siku mbili kwa wakristo Ulimwenguni kote kuazimisha siku ya kuzaliwa Bwana na Mwokizi wetu YESU KRISTO siku ambayo hujulikana kama Christmas, wenyeji wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini hasa Mkoani Kilimkanjaro wanako toka Wachaga na Wapare hii leo walimiminika kwa wingi katika misafara ya magari madogo binafsi wakielekea mwakao.
  Blogu hii, iliyokuwa njiani ikitoka Arusha ilishuhudia misafara hiyo ya magari yaliyojaa wanafamilia hao ikifukuzana kuwahi kupanda safu za milima ya Pare na Uchagani.
Kasi ya Mwaka huu kuongezeka kwa magari madogo barabarani inadaiwa kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma hasa kutokana na kero ya usafiri wa mabasi na ndege.
Askari wa usalama barabarani nao leo hii walikuwa katika mishe mishe zao kama kawaida kwa magari hayo mengi kusimamishwa na kufanyiwa ukaguzi wa hapa na pale na mambo mengine kuendelea.
Jambo kubwa na la kumshukuru Mungu ni kuwa  Blog hii katika pepesa pepesa ya jicho la kamera yake halikufanikiwa kuona ajali yoyote ya magari hayo wala mabasi zaidi ya magari kadhaa yaliyokutwa yakiwa yamechemka kutokana na kwenda umbali mrefu.
 Walichemka na kuamua nao kufanya mambo.
 Magari yaliendelea na msafara
 Mvua kidogo ilinyesha barabarani lakini haikuleta madhara
Vizuizi vya Polisi vilikuwepo njiani kuhakikisha usalama.
 Ni magari ya kila namna yalikuwepo.
Mambo ya namna hii ilikuwepo sana tu.
source father kidevu

No comments:

Post a Comment