Maafisa
wa kuzima moto wakiendelea na kuzima moto katika ghala moja lililolipuka
LagosMoto mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Nigeria Lagos.Taarifa
zinaarifu kuwa moto huo ulianza katika eneo la kuhifadhi baruti na kisha
kuenea kwa haraka katika majengo mengine yaliyo karibu na ghala hilo.
Moshi
mkubwa umeenea kote katika kisiwa cha Lagos na wazima moto wanajithidi
kuuzima moto huo.Bado baadhi yamajengo yanaendelea kuteketea.Mwandishi
wa BBC anasema maafisa wa kuzima moto walikuwa na wakati mgumu kufika
eneo hilo kutokana na idadi kubwa ya watu waliokuwa hapa.
Kwingineko,
maafisa wa usalama Kaskazini mwa Nigeria wanasema watu waliojihami kwa
bunduki wamefyetua risasi na kuwaua watu sita katika kijiji chenye idadi
kubwa ya wakristo.Msemaji wa jeshi ameiambia BBC, kuwa washambuliaji
hao waliwafyetua risasi waumini katika kanisa dogo wakati wa ibada ya
Krismasi.
Mshambuliaji
mmoja amezuiliwa na maafisa wa usalama katika eneo hilo.Ripoti zaidi
zinasema kuwa ulinzi umeimarishwa ili kuwaondoshea wasiwasi wakaazi wa
eneo hilo.
Hakuna
kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo katika jimbo la Yobe, lakini
kundi lenye itikadi kali za dini ya Kiislamu la Boko Haram limekuwa
likiwalenga Wakristo katika eneo hilo mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment