MTUHUMIWA
wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kujitegemea, Daud
Mwangosi kwa mara ya kwanza tangu alipofunguliwa kesi, jana alifikishwa
mahakamani akiwa katika gari la mahabusu (Karandinga), tofauti na awali
ambapo alikuwa akifikishwa kwa gari tofauti na wengine.
Pasificus Cleophace Simon (23) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Iringa kwa tuhuma ya kumuua mwandishi huyo katika hafla ya ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa, uliofanyika Septemba 2, mwaka huu.
Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC, linalosadikiwa kuwa ni la RCO na mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 Pick-Up akiwa katika ulinzi mkali, huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa, jambo lililozusha hisia tofauti miongoni mwa wananchi wengi mkoani hapa.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Adolf Maganda aliambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Dyness Lyimo kuwa, upelelezi haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Januari 3, mwakani 2013 itakapotajwa tena.
Desemba 6 mwaka huu, mtuhumiwa huyo hakufikishwa mahakamani kwa madai kuwa gari la kusafirishia mahabusu lilikosa mafuta.
Katika hali isiyo ya kawaida, mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 akiwa mahakamani hapo alipandisha hasira na kutaka kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti hili aliyekuwa akipiga picha mahakamani hapo.
Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema: “Watu tuna uchungu na kesi halafu wewe unapigapiga picha hapa kwa sababu gani, nitakumaliza mimi, alaa.”
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya CHADEMA.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments:
Post a Comment