MSANII
wa filamu nchini, Sajuki alidondoka jukwaani juzi wakati akijaribu
kuwasalimia mashabiki wake waliofurika kumtazama kwenye Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid, Arusha.
Sajuki
ambaye jina lake halisi ni Juma Said Kilowoko alikuwa akisumbuliwa na
matatizo ya kupungukiwa dawa na kulazimika kwenda kutibiwa nchini India.
Mwingizaji
huyo alipanda jukwaani katika tamasha la lililowahusisha wasanii wa
filamu na muziki, lakini ndoto yake ya kusalimia mashabiki wake
hakuwezekana.
Mara
baada ya kukabidhiwa kipaza sauti Sajuki alitamka neno moja ”ahhh" na
kudondoka chini na wasanii wenzake walimsaidia kuinuka na kumuondoa
jukwaani hapo.
Akizungumza
na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki alisema
hali yangu si nzuri kwani nahishiwa nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
endelea kutembeleahttp://www.dj-sek.blogspot.com
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa, sijisikii vizuri,” alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi.
Hata
hivyo, mashabiki wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na
hali hiyo na kushutumu wasanii walioamua kumtumia ili wapate fedha ihali
mwenzao ni mgonjwa.
“Hawa
watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu huyu mtu anaumwa, badala ya
kumwacha apumzike wenyewe wanamzungusha bila ya kujali afya yake,”
walisema mashabiki hao.
No comments:
Post a Comment