BAADHI
ya watumiaji wa simu za viganjani zenye televisheni ni miongoni mwa
watu watakaoathirika na uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa televisheni
ya mfumo wa analojia.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Mawasialiano nchini (TCRA), akitoa taarifa kuhusu
uzimaji wa mitambo hiyo ya analoji kwenda dijitali, kwa mkoa wa Dar es
Salaam, Injinia Endrew Kisaka alisema hali hiyo inatokana na simu hizo
kuunganishwa na mfumo huo.
Alisema
simu hizo zitakosa huduma hiyo ya matangazo hadi pale kampuni hizo za
simu kwa shirikiana na malaka hiyo kuzindua mfumo utakaokwenda sambamba
na dijitali hivi karibuni.
Injinia
Kisaka, alisema uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika haraka ili kuepusha
usumbufu unaoweza kujitokeza kwa watumiaji wa simu hizo.
Akifafanua
zaidi kuhusu changamoto kuhusu ving’amuzi, alisema endapo utatokea
usumbufu wananchi wasisite kurudi sehemu waliko nunua king’muzi hicho
kwa maelezo zaidi.
“Unajua
kuna baadhi ya maeneo kama vile yenye majengo marefu na mabonde ambapo
maeneo hayo hukosekana ‘signal’ sasa mkiona hivyo rudini kwa wauzaji
wenu wawape ushauri wa kitaalamu utakaosaidia kupata matangazo hayo kwa
ubora”alisema Kisaka.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Prof. John Nkoma alisema serikali
imejitahidi kuondoa kodi katika kuingiza ving’amuzi ambapo imesaidia
kupunguza bei na kuwa sh 39,000 ambayo anaamini kila Mtanzania atamudu
kukipata.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa ikitoa elimu kwaumma kwa
kiwango chakuridhisha,hivyo uhamaji hautakuwa na usumbufu kwa watumiaji
wa huduma za utangazaji.
Pamoja na hayo, alieleza mabadiliko hayo hayatahusu
utangazaji kwa satelaiti, waya (cable) na redio.
No comments:
Post a Comment