Yaw Berko |
SASA rasmi,
Yaw Berko amebaki historia ndani ya klabu ya Yanga. Hiyo inafuatia klabu ya St
Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuridhika naye baada ya
majadribio.
Katibu wa
Yanga, Lawrence Mwalusako ameiambia dj sek jana kwamba kipa huyo
Mghana amefuzu majaribio Lupopo na amesajiliwa moja kwa moja.
Kuondoka kwa
Berko, kunatoa nafasi kwa kiungo kutoka DRC, Kabange Twite kusajiliwa katika
klabu hiyo ya Jangwani, akiungana na kaka yake, beki Mbuyu Twite. Wachezaji
wengine wa kigeni wa Yanga ni kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na
washambuliaji Didier Kavumbangu kutoka Burundi na Hamisi Kiiza kutoka Uganda.
Berko
alijiunga na Yanga SC mwaka 2009, akitokea Liberty Proffessional ya kwao Ghana,
timu ambayo ilimuibua pia Michael Essein na nyota wengine kibao wa Ghana.
Aliletwa nchini na kocha wa zamani wa Yanga, Mserbia Kostadin Bozidar Papic
aliyewahi kupiga kazi Ghana katika klabu ya Hearts POf Oak.
Alikuwa kipa
bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Bara msimu wa 2010/2011 na katika kipindi chake cha
kufanya kazi Jangwani, anajivunia kuiwezesha timu kutwaa mataji ya ubingwa wa
Bara msimu wa 2010/2011 na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la
Kagame mara mbili mfululizo, 2011 na 2012.
2011 alidaka
mechi zote, lakini 2012 alidaka hadi Robo Fainali alipoumia na kumuachia Ally
Mustafa ‘Barthez’ aliyedaka hadi ubingwa. Yanga imeridhika na uwezo wa Barthez
langoni iliyemsajili kutoka Simba msimu huu na kuamua kuachana na Berko, ambaye
alikuwa kipenzi cha wapenzi wa klabu hiyo.
Awali, Yanga
ilijifikiria mara mbili kuachana na Berko, kwa kuhofia Barthez angeanza
‘kuwaringia’ kwa kuona amebaki peke yake kipa bora, lakini imepanga
kumhamasisha Said Mohamed kuimarisha kiwango chake, vinginevyo atatemwa
mwishoni mwa msimu.
Na Yanga
imekuwa na ‘jeuri’ ya kumtema Berko baada ya kuona mwakani haitashiriki
michuano ya Afrika, zaidi ya Ligi Kuu na jukumu la kwenda kutetea taji lake la
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda.
Japokuwa
anaondoka, lakini kwa uhodari wake langoni, Berko atabakia kwenye kumbukumbu ya
mashabiki wa Yanga.
WASIFU WAKE:
JINA: Yaw
Berko
KUZALIWA:
Oktoba 13, 1980
ALIPOZALIWA:
Accra, Ghana
KLABU ZA
AWALI:
Mwaka Klabu
2000-2005: Liberty Professional
2005-2006: Pisico Binh Dịnh F.C. (Vietnam, mkopo)
2006-2009: Liberty Professional
2009- 2012: Yanga
SC
2012: St Eloi Lupopo
No comments:
Post a Comment