Wachezaji wa kikosi cha Zambia wakitafakari wakati wakiwa mazoezini jijini Lusaka jana kabla ya kutua jijini Dar es Salaam leo (Desemba 19, 2012) ili kuivaa Taifa Stars katika mechi yao ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi. |
Katongo na wenzake |
Katongo akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili |
Katongo akizungumza na wanahabari baada ya kuwasili |
Wachezaji wa Chipolopolo wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere leo jioni |
Kocha Herve Renard akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutua Dar leo |
NAHODHA Christopher Katongo ambaye juzi aliwashinda Didier Drogba wa Shanghai Shenhua na Yaya Toure wa Manchester City na kutwaa Tuzo ya BBC ya Mwanasoka Bora wa Afrika ni miongoni mwa nyota wa mabingwa wa Afrika, Zambia “Chipolopolo” waliotua jijini Dar es Salaam jioni hii kwa ajili ya kucheza mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa “Taifa Stars” itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Katongo
na wenzake wametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere mishale ya saa 11:45, wakiwa pia na kocha Mfaransa Herve
Renard, ambaye ndiye aliyewasaidia kuishangaza dunia kwa kutwaa ubingwa
wa Afrika 2012 katika fainali waliyoshinda kwa penati dhidi ya Ivory
Coast nchini Gabon.
Mbali
na Katongo, nyota wengine waliotua leo ni pamoja nyota wa TP Mazembe ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rainford Kalaba na Given Singuluma
ambaye ni mfungaji bora wa fainali za kwanza za michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).
Wengine
ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick
Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde, Hichani
Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha,
Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford
Kalaba, Roderick Kabwe na Salulani Phiri.
Hata
hivyo, beki Stopilla Sunzu wa klabu ya TP Mazembe ambaye ni mshindi wa
Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mwaka 2012,
si miongoni mwa wachezaji waliotua nchini jioni hii, leo Desemba 19,
2012 na kocha Renard amesema atakuja kivyake kwani ameenda Accra, Ghana
kushiriki katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Mwanasoka Bora wa Afrika
zinazoandaliwa na Shirikishon la Soka (CAF).
Sunzu anawania Tuzo ya Mwansoka Bora miongoni mwa nyota wa Afrika wanaocheza ligi za ndani.
Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Katongo alisema kuwa Stars imezidi kuimarika katika siku za hivi karibuni na kucheza soka safi; hivyo hawatarajii kupata mteremko.
Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Katongo alisema kuwa Stars imezidi kuimarika katika siku za hivi karibuni na kucheza soka safi; hivyo hawatarajii kupata mteremko.
“Tunashukuru
sana kupata mwaliko wa kuja kucheza Tanzania… nadhani itakuwa mechi
yenye ushindani mkali. Tumejiandaa vizuri maana tumeiona timu ya
Tanzania ikicheza soka safi na kuzipa shida timu kubwa barani Afrika,”
alisema Katongo.
“
Sisi ni mabingwa wa Afrika na hivyo wengi wanatuangalia kuona tutafanya
nini mwaka huu baada ya mwaka uliopita kufanya vizuri sana.
“Tunahitaji
kujiandaa vizuri zaidi ili kutetea ubingwa wetu na mechi hii (dhidi ya
Stars) ni sehemu mojawapo ya maandalizi yetu,” alisema Katongo, mshindi
wa Tuzo ya BBC ya Mwansoka Bora wa Afrika 2012.
Kocha
aliyeisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa fainali zilizopita za Afrika
(Afcon 2012) zilizofanyika Equatorial Guinea na Gabon mwanzoni mwa mwaka
huu, Herve Renard,alisema vilevile kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kwao
kwa sababu Tanzania inakuja juu kisoka.
“Tanzania kwa sasa inacheza soka safi na si timu ya kubeza hata kidogo. Tunafurahi kupata mwaliko wa kuja kucheza nao,” alisema.
“Mechi
hiyo ni sehemu ya maandalizi yetu kuelekea kwenye michuano mikubwa
inayotukabili (fainali za Afcon 2013)… tutaonyesha soka zuri, alisema.
“Kikosi
tulichokuja nacho kina asilimia 60 ya wachezaji ambao walishiriki
katika kutwaa ubingwa wa Afrika. Naamini tutafanya vizuri,” aliongeza
Renard mwenye umri wa miaka 43.
Akieleza
zaidi, kocha huyo alisema kuwa nyota wake mwingine, beki Stopilla
Sunzu wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
atakuja peke yake baadaye kwa sababu ameenda nchini Ghana kuhudhuria
utoaji wa Tuzo za Wanasoka Bora wa Afrika Mwaka 2012 zilizoandaliwa na
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
KIINGILIO
Katibu
Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa kiingilio cha chini katika
mechi hiyo ya Jumamosi itakayoanza saa 10:00 jioni kitakuwa Sh. 5,000
wakati cha juu kitakuwa Sh. 30,000.
No comments:
Post a Comment