Pages

Wednesday, January 23, 2013

CUF YATOA ONYO KAZI KWA WAZIRI MUHONGO JUU YA GESI ASILIA YA MSIMBATI MKOANI MTWARA

.



CHAMA Cha Wananchi (CUF)  kinamuonya Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo na kumtaka atambue kuwa katika suala hili la Gesi, wananchi wa Mtwara ndiyo watashinda na Gesi lazima inufaishe taifa ikiwa palepale Mtwara na hakuna haja ya kuendelea kuwaonea wananchi wa mikoa ya pembezoni kwa kisingizio cha kulinda mshikamano wa kitaifa.
Akizungumza na mkoani Mtwara Naibu Katibu Mkuu Julius Mtatiro,Kuta alisema kuwa kunamshikamano gani wa kitaifa Mtwara ikiwa mikoa ya kusini inashughulikiwa na serikali ya CCM kila kukicha.
 
Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo.

"Wameshughulikiwa kwenye korosho na kuacha mkulima wa korosho awe masikini huku Matajiri wachache wanaoikusanya wakitajirika na kutoa 10% kwa viongozi wa CCM, wamewashughulikia wakulima wa ufuta na hivi sasa hawana mbele wala nyuma. Hata gesi nayo lazima ije DSM ?.

Ya songosongo inatosha kuja DSM, hii ya Mnazi Bay iachwe"alisema Mtatiro

No comments:

Post a Comment