Pages

Thursday, January 24, 2013

GODBLESS LEMA AFUNGA SHULE, MKUU WA WILAYA AAMURU IFUNGULIWE MARA MOJA



DSC00054
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela  amesema kuwa wanasiasa wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kukomea kwenye madaraka yao na wala sio kujivisha
madaraka ambayo si yao kama ilivyotokea katika shule ya sekondari
Korona ambayo ilifungwa jana na mbunge wa Arusha Mjini
Hatua hiyo imekuja leo mara baada ya Mbunge huyo kufungia shule ya
sekondari Korona kwa madai kuwa shule hiyo badala ya kuwasaidia
wanafunzi inawatesa na hivyo haina maana ya kuwepo

Mongela aliyasema hayoleo mjini hapa mara baada ya kutembelea rasmi
shule ya sekondari Korona ambayo ilfungwa na Lema na kudai kuwa Mbunge
huyo hajawatendea haki wanafunzi kwa kuwambia kuwa wanatakiwa kufunga
shule mpaka changamoto zitatuliwe tena kwa haraka sana
Mongela alisema kuwa endapo kama wanasiasa watakuwa wanajichukulia
hatua na kutangaza kusitishwa kwa huduma ya elimu basi wimbi kubwa
sana la vurugu litatanda ndani ya mkoa wa Arusha hivyo wanasaisa
waachane na mtikisiko huo ambao umetokea katika shule ya sekondari
Korona
Kutokana na Kauli hiyo ya Mbunge Lema ya kufunga shule hiyo alidai
kuwa wanafunzi wote wanatakiwa kuhudhuria shule tena jumatatu asubuhi
na kama hawatafanya hivyo basi sheria itachukua mkondo wake ikiwa ni
pamoja na kuwahoji wazazi ambao hawawaruhusu wanafunzi kurudi
mashuleni
Pia aliutaka uongozi wa jiji la Arusha kuhakikisha kuwa linamvua cheo
mkuu wa shule hiyo mara moja sanjari na kutatua matatizo ya shule hiyo
ndani ya masaa 48 na kama hawatafanya hivyo basi watavuliwa uongozi na
madaraka yao kwani anachokilalamikia Lema ni kweliNaye Lema alisema kuwa anachokitafuta machoni mwa watu na Mungu ni
haki na wala sio sifa kwa kuwa alipofunga shule hiyo alikuwa na
viongozi wa Serikali,kama Vile Afisa elimu Sekondari,Afisa utumishi
na kwa hali hiyo ni vema kama Jiji likasaidia  na kutatua changamoto
ambazo zimo kwenye shule za Kata

No comments:

Post a Comment