Na Francis Godwin
Jinamizi
la ajali limeendelea kuwaandama viongozi wa juu serikali na vyama
baada ya juzi waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa kunusurika kifo katika
ajali iliyotokea eneo la Bwawani mkoani Morogoro ,Mkuu wa jeshi la
polisi nchini (IGP ) Said Mwema leo amenusurika kifo baada ya gari
lake alilokuwa akisafiria kupinduka.
Ajali
hiyo imetokea majira ya mchana katika eneo Mkundi Manispaa ya
Morogoro wakati kiongozi huyo akitokea jijini Dar es Salaam kwenda
mkoani Dodoma.
Hata
hivyo katika ajali hiyo hakuna madhara makubwa kwa binadamu zaidi ya
gari kuharibika kiasi na msafara wa IGP kuendelea na safari ya
Dodoma kwa kutumia usafiri mwingine .
No comments:
Post a Comment