Magari yakiwa yanateketea kwa moto mkoani Mtwara.
Nyumba ikiteketea kwa moto mkoani Mtwara hii leo katika vurugu zilizozuka.
WATU
watatu wamefariki dunia Mkoani Mtwara baada ya kutokea vurugu kubwa kati
ya Askari wa Jeshi la Polisi na waendesha Pikipiki maarufu (Bodaboda).
Taarifa
za tukio hilo zilizotufikia hivi Punde zinadai kwamba vurugu hizo
zimesababishwa na Askari Poli kumkamata mmoja wa dereva bodaboda hao na
kuanza kumpiga kiasi cha kupoteza fahamu.
Mbali
na watu hao waliouwawa katika vurugu hizo taarifa hiyo pia imeeleza
kuwa zaidi ya nyumba na ofisi tatu za serikali pamoja na magari matano
yamechomwa moto.
Tunaendelea kuzifuatia taarifa hizo kwa kina na tutaendelea kuwajulisha hivyo endeleeni kufuatilia kwa undani wake.
Chanzo Habarimpya.com
No comments:
Post a Comment