Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 16, 2013

TAZAMA POLISI AKIPEWA KIPIGO KIKALI KWENYE MAANDAMANO YA WANACHUO WA IFM



Jeshi la Polisi linaonekana kufanya kazi zaidi kwa mazoea kuliko kuzingatia mafunzo wanayopewa, pichani ni askari polisi aliyejeruhiwa na wenzake baada ya kupigwa marungu kwa kutomjua kama nayeye ni askari hadi alipopiga kelele ‘mtaniua mimi mwenzenu’ ndipo wakamuachia.
Kilichofuata baada ya askari huyo kuachiliwa na wenzake alimalizia hasira zake zote kwa wanafunzi hao kwa kutembeza kipigo (mkong’oto) mkali kwa wanafunzi Chuo Cha IFM waliojaribu kutaka kulazimisha jeshi la polisi kufanya mkutano mbele ya kituo cha Polisi Kigamboni badala ya kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava Kigamboni bila kujali kuwa wanafunzi hao walikuwa wakikabiliana na moshi nzito wa mabomu ya machozi lakini pia walisha kuwa chini ya ulinzi mkali na hakukuwa na sababu yeyote ya kuwapiga hivyo.
Mbali na askari huyo kulikuwepo na askari wengine wawili akiwemo mmoja wakike naopia waliambulia kipigo hiko. Fuatilia picha za Askari huyo na matukio aliyofanya .
Picha hii inakuonesha kwa karibu namna rungu lilivyompasua Askari huyu, hapa utapata picha kama huyu askari aliyepigwa kidogo tu baadaye akaachiwa ameumia hivi je wale waliopata mkong'oto wapo kwenye hali gani.
Hapa anazuia damu sehemu aliyopigwa isindelee kuvuja kwa kutumia kitambaa.
Baada ya kupata nafuu anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi huyo

Hakuishia hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na kumpa kipigovile alivyojiskia ili amalizie hasira zake.
Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa.
Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka!
BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko. 
 
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza fahamu. 
 
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
Askari Polisi ambaye hakuwa kwenye sale za jeshi hilo akimsulubu mmoja wa wanafunzi wa IFM baada ya kudhibitiwa kwenye eneo la kituo cha Polisi Kigamboni walipofika kutaka kulazimisha kufanyika mkutano wao na kamanda Kova badala ya eneo lililopangwa kwenye viwanja vya Machava. Wanafunzi hao walikamatwa baada ya kupigwa mabomu ya machozi kwenye eneo hilo na kukamatwa kama kuku wa mdondo.
Askari wa kike na wakiume wakimdhibiti kwa bakora na marungu mwanafunzi wa chuo cha IFM (mwenye nguo za blue) baada ya kumchomoa kwenye jengo alilojificha ili kukwepa mabomu ya machozi.
Kundi la wanafunzi walishikwa kama kuku wa mdondo baada ya kupigwa mabomu ya machozi na kujikuta wakijificha sehemu moja kundi zima hali iliyosabisha kutembezwa kichurachura hadi kwenye kituo cha Polisi cha Kigamboni.
Mwanafunzi huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi.
Mwanafunzi huyu alidondoka kwenye Difenda baada ya Defenda hilo kujazana wanafunzi wengi ambao wakipelekwa kwenye kituo cha Polisi Kigamboni.
Baada ya kitikisa mabomu yakutosha kwenye baa pembeni ambako walijificha wanafunzi hao walitaka amani itawale huku wakikimbilia gari la polisi ili wajisalimishe.
Huyu alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga.
Hapa amri ilikuwa ni mwendo wa kutembea kwa magoti lakini kipigo cha bakora kililazimisha wengine kuwaruka wenzao ama kuwakanyaga wale waliochini.
Huyu hakujiweza kabisa mabomu yalimchanganya na kudondoka toka kwenye Difenda ya Polisi.
Virungu vilitumika kushindilia watu kwenye Difenda.
Hiki ndicho kikosi Kamili kilichotumia dakika 15 kusambaratisha kundi la wanafunzi zaidi ya 800 walioweka kambi ya muda mfupi kwenye kituo cha Polisi Kigamboni . Picha zote na Saidi P

No comments:

Post a Comment