SHIRIKA
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na Kampuni ya Wings of
Kilimanjaro ya nchini Australia, wameandaa safari ya kupanda Mlima
Kilimanjaro itakayowashirikisha watalii zaidi ya 100 ambao watashuka
toka kwenye kilele cha mlima huo kwa kutumia miavuli maalumu.
Aidha,
shughuli hiyo inayotarajiwa kukusanya dola milioni moja (sh bilioni 1.5)
ambazo zitatumika kusaidia miradi ya wananchi wanaoishi kuzunguka
hifadhi mbalimbali za taifa nchini.
Wakizungumza
na waandishi wa habari jijini hapa juzi, Meneja Uhusiano wa Tanapa,
Pascal Shelutete na Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Adrian Mgrae, walisema
fedha hizo zitaelekezwa kwenye miradi mbalimbali ya kukabiliana na
umaskini vijijini, uharibifu wa mazingira na misaada ya kibinadamu.
Walisema
misaada hiyo inajumuisha uchimbaji wa visima vya majisafi ya kunywa,
kuboresha miundombinu ya elimu na kusaidia waathirika wa ukimwi,
ikisimamiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya One Foundation, Plant
with Purpose na Worldsave International.
No comments:
Post a Comment