Pages

Monday, January 7, 2013

YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI BAADA YA KUTOKA SARE NA TIMU ILIYOTOKA KUWAFUNA BAYERN LEVEKURSEN KWENYE KOMBE LA UJERUMANI



Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football
Kikosi cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ambao uliishia kwa sare ya bao 1-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Adora football Belek - Antalya.

Kocha Brandts ameendelea kukifua kikosi chake na kufanyia marekebisho ya baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ambao hata hivyo Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo.
Arminia Bielefeld ambao awali hawakutegemea Tanzania kuwa kunaweza kuwa na timu ambayo inaweza kuwapa upinzania, walikiri mwishoni mwa mchezo kwamba Yanga ina timu nzuri na hawak.utegemea kuona kiwango kizuri cha mchezo kilichoonyeshwa na vijana na wa Jangwnai alisema mmoja wa maofisa wa Arminia Bielefeld.
Ukizingatia Armini Bielefeld ilikuwa imetoka kuifunga Bayern Levekursen 4-2 katika mchezo wa kombe la Ujerumani, walikutana na vijana wa Jangwani ambao waliweza kuutawala mchezo huo kuanzia kwa mlinda mlango Ally Mustafa 'barthez, mpaka kwa washambuliaji wake.
Nahodha wa Young Africans Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto akisalimiana na wamuzi wa mchezo na nahodha wa timu ya Arminie Bielefeld kabla ya mchezo huo jana
Brandts alisema amefarijika na matokeo ya mchezo huo, japokuwa lengo lake kubwa lilikuwa ni kupata ushindi katika mchezo huo lakini wachezaji wake waliweza kufanya kazi nzuri sana uwanjani kitu kilichofanya Wajerumani kushangaa.
Young Africans mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, jioni itakua ikifanya mazoezi ya kujenga mwili misuli (GYM) katika  Hotel ya Fame Residence Lara & Spa ambao kesho asubuhi itaendelea na mazoezi katika viwanja vya Fame Residence 
 PICHA na habari kutoka mtandao wa yanga

No comments:

Post a Comment