Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Aden Rage alisema
jana kuwa kuteuliwa kwa wachezaji hao kumetokana na viwango vyao na umri
na endapo watafuzu, basi watacheza soka klabu hiyo ya England yenye
historia kubwa nchini humo.
Rage alisema kuwa wameingia kwenye makubaliano
maalumu na timu hiyo katika kuendeleza upande wa ufundi, uongozi na timu
kwa jumla na hilo limetokana na historia ya Simba SC ambayo miaka ya
1960 ilikuwa inajulikana kwa jina hilo.
Alisema kuwa hatua hiyo ni faraja klabu ya Simba
kutokana na ukweli kuwa matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa kama
yalivyo kwa timu hiyo ya England.
Aliongeza kuwa wana mawasiliano mazuri na mmiliki na mwenyekiti wa timu hiyo, Ellis Short kuhusiana na mpango huo.
“Tumeweka mikakati mikubwa na kuhakikisha Simba
inafikia hatua kubwa ya maendeleo. Tunaendelea na mazu ngumzo na
viongozi wakuu wa timu hiyo na mwezi ujao, tuta kwenda huko kufanya mazu
ngumzo zaidi na kukamilisha masuala mbalimbali,” alisema Rage.
Ujumbe huo utaongozwa na Rage na wengine watakaojulikana hapo baadaye. Safari hiyo itafanyika wiki ya kwanza ya mwezi Machi.
Aidha, Rage alisema kuwa katika kuhakikisha
ushirikiano wao unadumu, klabu hiyo itavaa jezi zenye nembo ya timu ya
Sunderland kuanzia msimu ujao. Alisema kuwa ili kuondoa mtafaruku, jezi
hiyo pia itakuwa na nembo ya wadhamini wao we ngine.
Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya klabu ya Simba, Rahma
Al Haroos jana alikabidhi jezi mpya kwa klabu hiyo kwa ajili ya
kutumika kesho katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya timu
ya Recreative de Libolo ya Angola.
Alharoos alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi jezi hizo ni kuongeza morali kwa timu hiyo ili kushinda mechi hiyo.
Wakati huohuo Rage amesema kuwa fedha za ma lipo
ya awali ya mchezaji wao, Emmanuel Okwi aliyeuzwa klabu ya Etoile du
Sahel ya Tunisia hazijawafikia mpaka sasa. Etoile du Sahel ilimnunua
Okwi kwa dola za kimarekani 300,000 (Shs 470 milioni).
Alisema kuwa timu hiyo ya Tunisia imeahidi kulipa kwa mikupuo miwili.
No comments:
Post a Comment