skip to main |
skip to sidebar
JAMALI MALINZI AUNGURUMA JIJINI DAR LEO KUHUSU KUNG'OLEWA KUGOMBEA URAIS TFF.
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya
Urais wa TFF kabla ya kuenguliwa na kamati ya uchaguzi ya TFF,Jamali
Malinzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
kuhusu hatua ya kuondolewa kwenye mchakato huo, ambapo alipinga kabisa
hatua hiyo ya kuondolewa. Hata hivyo amemtaka Rais Tenga kumaliza vizuri
kazi yake ambayo ameifanya kwa ufanisi wa hali ya juu kwa kulimaliza
suala hili bila ya mgogoro zaidi.
Waandishi wa habari mbalimbali waliojitokeza kwenye mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Sababu
zilizotolewa na kamati ya uchaguzi ya TFF ni uzoefu wa miaka mitano,
Tuhuma za kupinga waraka wa kubadili katiba ya TFF baada ya kuwekewa
Pingamizi iliyowekwa na Agape Fue ambaye, alikata rufaa kwenye kamati ya
rufaa ya TFF kupinga kuto tendewa haki.
Alihoji
kuwa huyo agape fue ni mwanamke au mwanaume kwasababu hajawahi kutokea
kwenye kamati ya uchaguzi ya TFF wala kamati ya rufaa.
No comments:
Post a Comment