Wasira akisaini kitabu cha waombolezaji kwa niaba ya Rais
RAIS
Jakaya Kikwete ametoa rambirambi kufuatia kifo cha muasisi wa TANU/CCM
na mzalendo wa kwanza kuwa mkuu wa Kanisa la KKKT- Dayosisi ya kati
kutoka kwa wamisionari, mchungaji Thomas Musa(86). Marehemu Thomas Musa
aliyezaliwa desemba 6,1927 wilayani Iramba alifariki ijumaa iliyopita na
kuzikwa jumanne wiki hii, kijijini kwake Kinampanda, Iramba, mkoani Singida.
Katika
salamu zilizotolewa jana jumatano jioni nyumbani kwa marehemu na waziri
wa nchi ofisi ya Rais Stephen Wasira, Rais amesema amesikitishwa sana na
kifo hicho kutokana na mchango wa marehemu kwa taifa, hasa elimu na
afya katika uhai wake.
Rais
alisema CCM na Serikali yake inaungana na familia ya mjane na mtoto wa
marehemu Jaji Kipenka Musa anayesimamia familia hiyo, katika kipindi
hiki kigumu cha majonzi.
Katika
rambirambi hiyo ambayo hakutaka itangazwe, Rais amesema ingawa mzee Musa
amefariki, lakini matendo yake daima yataendelea kukumbukwa na kuenziwa
kwa ajili ya maendeleo ya taifa
No comments:
Post a Comment