Askofu
mkuu wa Canterbury amesema amazipokea taarifa za kujiuzulu kwa Papa
Benedict wa XVI kwa huzuni mkubwa ingawa anaelewa undani wa hatua yake,
kiongozi wa Ujeremani Angela Merkel amesifu mchango wa Papa wa
kupendekeza mjadala wa makanisa, waislamu na wayahudi.
Kasema
uamuzi na hatua ya Papa Benedict XVI kujiuzulu mwishoni mwa mwezi huu
baada ya takriban miaka minane kuliongoza Kanisa Katoliki kwa hoja kuwa
umri wake wa miaka 85 ni mkubwa kiasi kwamba hawezi kuendelea kuhudumu
zaidi ya umri huo, ni sahihi
Makao
makuu ya Kanisa Katoliki huko Vatican yanasema yanatarajia Papa mpya
atachaguliwa kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu na sherehe za Pasaka
ambapo kama hufahamu, tabia ya kujiuzulu kwa Papa si ngeni, ingawa ni
tukio jipya katika karne za hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment