KLABU ya soka ya Simba inasikitika kutangaza kifo cha mjumbe wake wa Kamati ya Mashindano na Maendeleo ya Timu za Vijana, Hamis Mrisho maarufu kwa jila la Hamis Dalali aliyefariki dunia alfajiri ya leo kijijini kwake Matimbwa, Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti
wa Simba, Alhaji Ismail Aden Rage, amesema msiba huo ni mzito sana kwa
klabu na kwamba katika mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom, wachezaji
na viongozi wa Simba watavaa vitambaa vyeusi kuashiria msiba huo mzito.
"Kwa
niaba ya klabu ya soka ya Simba na kwa niaba yangu binafsi, naomba
kutoa salamu zangu za rambirambi za dhati kabisa kwa familia, ndugu,
jamaa na marafiki wa marehemu kutokana na kifo cha ghafla ndugu Mrisho.
Nilimfahamu kama mchapakazi wa kweli na mtu aliyeipenda Simba kwa moyo
wake wote," alisema Rage.
Mrisho
ambaye pia alikuwa Katibu wa Matawi ya Simba Wilaya ya Kinondoni,
alikuwa ni mtu aliyekuwa akijituma sana kufanya kazi zozote za klabu kwa
kadri ya maelekezo ya uongoz na hakuwa na makundi huku akipendwa na
watu wote waliokuwa wakimfahamu.
Marehemu
alizaliwa mwaka 1965 na ameacha mjane na watoto wanne. Mazishi yake
yanatarajiwa kufanyika leo jioni huko Matimbwa, Bagamoyo.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMEN.
Imtolewa na
Ezekiel Kamwaga
No comments:
Post a Comment