MAMLAKA
ya Mapato Kenya(KRA), inamshikilia mwandishi wa habari wa Tanzania kwa
tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin kiasi cha kilo
5.436 zenye thamani ya karibu Sh234 milioni.
Mtanzania
huyo ambaye aliwahi kuwa mtangazaji katika kituo kimoja cha redio
nchini, alikamatwa akiwa anataka kusafirisha dawa hizo kwenda China.
“Mamlaka
ya Mapato Kenya inataka kutaarifu maendeleo ya sakata la kukamatwa kwa
kilo 5.436 za heroin zilizokamatwa Januari 23 mwaka 2013 saa 4:40
usiku.”
“Imethibitika
kuwa kilichokamatwa ni dawa aina ya heroin yenye thamani ya Sh13
milioni za Kenya…kwamba mtuhumiwa… (Jina tunalo kwa kuwa hajafikishwa
mahakamani) hakuwa mwanafunzi lakini ni mtangazaji wa redio nchini
Tanzania.”
Ametambulika
kuwa mtangazaji wa kituo kimoja cha redio kwa tuhuma za kusafirisha
dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya Sh234 milioni.
Mtuhumiwa
huyo alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenyatta akiwa
katika jaribio la kuelekea nchi za Ulaya na kwamba kukamatwa kwake
kulifanikiwa kutokana na mtego ulioandaliwa na maofisa wa usalama
uwanjani hapo.
Taarifa
zinasema kuwa, mtuhumiwa huyo alijitambulisha kama mwanafunzi anayesoma
Sweden, lakini hata hivyo ilikuja kubainika kuwa alikuwa na kibali cha
ukazi alichokipata Novemba 28 na kilitazamiwa kuisha muda wake Novemba
28,2014.
Naibu
Kamishna wa KRA, Kenned Onyonyi alisema kuwa maofisa wa usalama
wanaendelea na uchunguzi zaidi na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Habari
zinasema kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na raia
mmoja wa Sweden, ambaye alimtambulisha kwa maofisa usalama kwamba
amekuwa akisafiri mara kwa mara katika nchi za Ghana, Kenya na
Mauritius.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa huyo amewahi kufanya kazi na Clouds fm
akiwa kama mtangazaji mwanafunzi katika kipindi cha Leo tena na baadaye
aliachana na kampuni hiyo na kujiunga na gazeti hili akiandika habari za
burudani. Aliachana na gazeti hilo na kuendelea na maisha yake ya
kawaida.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini,
Godfrey Nzowa alisema kuwa hawajapata taarifa za kukamatwa kwa
Mtanzania huyo, bali wamezisoma tu kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
“Kuna
utaratibu ambao inabidi watujulishe kwani kuna tume ya kuratibu dawa za
kulevya hivyo tunasubiri atuambie kuhusu tukio hilo,”alisema Nzowa.
No comments:
Post a Comment