Pages

Monday, February 11, 2013

MWANAMKE ATIMULIWA KWA KUTUHUMIWA NI MCHAWI ILOLO MBEYA



Zainabu Zuberi mwenye kitambaa cheusi kichwani akiongozana na askari kanzu pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuokolewa na askari hao eneo la tukio ili asishambuliwe na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa ni mchawi


Zainabu Zuberi akituhumiwa kuhusika na ushirikina.


 Mume wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza udini na kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani hapo.

Moja ya askari akipata maelezo kwa mama aliyepotelewa na mtoto wake katika mazingira ya kutatanisha wiki mbili zilizopita mpaka sasa hajapatikana mtoto huyo





Wananchi hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo katika mkutano ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na hali hiyo.


Hii ndiyo nyumba anayoishi anaetuhumiwa kwa uchawi ilolo Mbeya


 Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.


Wananchi wa Mtaa wa Ilolo Kata ya Manga Jijini humo kumfukuza mtaani hapo Mwanamke anaye fahamika kwa jina la Zainabu Zuberi akituhumiwa kuhusika na ushirikina.

Wananchi hao ambao awali walitaka kujichukulia hatua mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba yake mtuhumiwa huyo walidai kuchoshwa na maovu yanayofanywa na mwanamke huyo.
Baadhi ya matendo ya kishirikina wanayomtuhumu mwanamke huyo kuhusika nayo ni pamoja na kujigamba kuwamaliza wanakijiji hao kwa kuwaloga ikiwa ni pamoja na kuwaloga watoto wao kitu ambacho wanasema kimeshatokea.
Wamedai kuwa mwanamke huyo amekuwa akiwagusa wanawake wajawazito na mimba zao huharibika ambapo pia wanafunzi wanaotoka katika mtaa huo wakifika Shule hushindwa kuona kabisa matukio ambayo mwanamke huyo anahusishwa.
 
Walisema mwanamke huyo anatuhumiwa kujihusisha na matukio ya kishirikina tangu ahamie mtaani hapo takribani miaka mitatu ambapo walisema wakazi hao walimwonya mapema kuhusu tabia hiyo baada ya kufuatilia historia ya maeneo aliyowahi kuishi.
 
 
Kwa upande wake Mume wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza udini na kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani hapo.
Rubea ameongeza kuwa mtaani hapo hawapendi mtu wa dini ya nyingine kujenga eneo hilo jambo ambalo lilipingwa vikali na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kumjadili mtuhumiwa huyo.
Awali mume wa mtuhumiwa huyo alikiri kuhama nyumba na mitaa zaidi ya kumi ambapo lisema maeneo mengine alikuwa amejenga lakini sehemunyingine alikuwa amepanga tu ingawa aligoma kusema sabbu inayomfanya ahame maeneo hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.
Amesema baada ya kuona wanachi wamepagawa na kutaka kujichukulia hatua mkononi ili mlazimu kuitisha mkutano wa hadhara ikiwa na kuitaarifu jeshi la polisi ambalo lilifika mapema eneo la Mkutano na kwatuliza wananchi wasifanye lolote ambapo Askari hao waliondoka na mtuhumiwa.
Aidha katika mkutano huo wananchi hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo katika mkutano ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na hali hiyo.
Matukio kama hayo yanayoashiria vitendo vya kishirikina ni pamoja na tukio la hivi karibuni la watu wawili kuzikwa wakiwa hai wakituhumiwa kuhusika na vitendo hivyo viovu ndani ya jamii.
 Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment