KATIKA
hali ya kawaida, tumezoea kuona watalii kutoka mataifa mbalimbali
duniani wakija nchini kuangalia vivutio vya utalii vilivyopo.
Baadhi ya vivutio hivi ni Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, majengo ya kale, mapango na nyumba za kihistoria.
Hata
hivyo, kumeibuka aina mpya ya utalii, unaojulikana kama utalii wa ngono,
ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi watalii wanawake wanaofuata
wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
Uchunguzi
uliofanywa na Mwananchi Jumapili, unaonyesha kuwa utalii huo
unaongezeka kwa kasi hasa katika maeneo yenye vivutio vingi vya utalii
ikiwamo Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar.
Imebainika
kuwa katika utalii huu, wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya
miaka 60 hadi 80 kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa
lengo la kutafuta vijana wa kiume wa kustarehe nao.
Uchunguzi
huo unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri
vinavyopendwa na wanaume huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri
kuja Tanzania kutafuta mwanamume atakayestarehe naye kingono.
Hali hiyo
inawakumba zaidi wanawake wanene, ambao kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo
kulazimika kusafiri kuja Afrika Tanzania ikiwamo kutafuta mwenza wa
kustarehe nao.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, utalii huu umeshamiri nchini,
ambapo vijana wa Kitanzania wanaufahamu na kukiri kuwa umewanufaisha na
baadhi yao kuwasaidia kupata tiketi za kwenda kuishi Ulaya.
Katika
Visiwa vya Zanzibar utalii huo unafanyika zaidi katika fukwe za Nungwi,
Kiwengwa, Paje, Kendwa, Jambiani na maeneo mengine yaliyopo pembezoni
mwa bahari.
Katika fukwe hizo vijana maalumu kwa kazi hiyo, wana kauli mbiu yao inayosema:“apewe mpaka apagawe, atoe tiketi.”
Kwa kauli
mbiu hiyo vijana hao wanamaanisha kuwa, kwa kila mwanamke
watakayekutana naye, watatumia kila mbinu ili kumfurahisha hadi
awasafirishe au kwenda naye Ulaya.
Abdulla
Ali Haji (Sio jina halisi) ni miongoni wa vijana wanaojihusisha na aina
hiyo ya utalii, akiishi visiwani humo ambapo anaeleza kuwa shughuli yake
kubwa ni kuzunguka katika fukwe mbalimbali akiwinda wanawake wa kizungu
wanaotaka kustarehe.
No comments:
Post a Comment