Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 1, 2013

SIASA:WABUNGE WA UPINZANI WATOKA NJE YA UKUMBI



Leo hii, Wabunge mbalimbali, miongoni mwao wa kutoka CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kuikataa hoja ya Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ya iliyomtaka
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuwasilisha nakala za Mtaala wa  Elimu za mwaka 2005.

Mitaala hiyo iliombwa tangu kikao cha Bunge lililopita na serikali iliahidi kuileta bungeni lakini baada ya Mh. James Mbatia kuombwa ahitimishe hoja yake binafsi na kukumbushia ahadi hiyo na kisha kuiomba serikali kuigawa mitaala hiyo kwa wabunge, Naibu Spika Job Ndugai alisema atatafakari ombi hilo na akiona linafaa, ataitaarifu Serikali na kuileta Bungeni. Akamtaka Mhe. Mbatia ahitimishe hoja yake.

Mbatia akaomba aliomba mwongozo wa Spika lakini ghafla Naibu Spika alimwabia muda wanaoutumia kuombea miongozo ndio muda wake wa kuhitimisha hoja.

Mbatia akalieleza Bunge kuwa jana alimwandikia Waziri wa Elimu kuwa anaiomba Mitaala hiyo lakini hakupata jibu, alishakwenda Wizara ya Elimu kuomba mitaala hiyo lakini hakupewa, ndipo alipohoji, “ikiwa Mbunge anadanganywa kiasi hiki itakuwaje kwa Mtanzania wa kawaida?”

Wabunge wa CHADEMA waliungana na wale wa NCCR-Mageuzi katika kuibana serikali. Naibu Spika, Ndugai aliwakwepa na kusema yeye ndiye mwenye maamuzi ya kuiomba serikali au la.

Ndugai akahitimisha hoja ya Mbatia na kutoa fursa ya kusikilizwa kwa hoja ya Dk Hamisi Kigwangallah, ndipo wabunge wa walipoamua kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.


No comments:

Post a Comment