Pages

Wednesday, March 13, 2013

Anorld Kayanda Kavunja Ukimya Kuhusu Kutosikika Tena Clouds FM



 Baada ya Anorld Kayanda kutosikika Redioni kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa na Maswali mengi juu ya hilo..Leo ameamua kuweka wazi kwa kupitia facebook Page yake na kuandika Haya:

"Napenda kutumia nafasi hii kwa namna ya pekee kabisa kuzungumza na Marafiki ambao mara zote mmekuwa mkiuliza juu ya ukimya wangu Redioni. Jibu ni fupi kabisa,imetokana na Maamuzi yangu ya KUREJEA MASOMONI hali ambayo kwa bahati nzuri imepewa Baraka na Viongozi wangu. Pengine hutanisikia Redioni lakini Mchango wangu wa namna mbali mbali utaendelea kuhifadhi hadhi ya U-Super Brand wa Clouds Media Group. Masomo yameweza kuiingilia Kazi yangu lakini kamwe hayataweza kuutenganisha urafiki wangu na nyinyi. Tuendelee kuwasiliana hapa na katika Twitter @arnoldkayanda au kwa namna yoyote tutakayojaliwa. Bless"

No comments:

Post a Comment