Pages

Sunday, March 17, 2013

Mama auawa kwa kupigwa shoka na mwanawe



Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile
Watu watatu wamefariki dunia mkoani Morogoro katika matukio tofauti akiwemo mama aliyeuawa na mwanaye na watoto wawili kuliwa na mamba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema katika tukio lililotokea Machi 14, mwaka huu, majira ya jioni huko Chamwino Manispaa ya Morogoro, mwanamke mmoja Dorcas Lugano (55) aliuawa kwa kupigwa shoka ubavuni baada ya kumtaka mwanaye akatafute kazi ili aanze kujitegemea baada ya umri kuwa mkubwa.

Awali mwandishi wa habari hizi alifika eneo la tukio na kushuhudia umati mkubwa wa watu waliofika eneo hilo kushuhudia mauaji hayo, ambapo baadhi ya waliohojiwa walidai kabla ya tukio hilo, kuliibuka ugomvi baina ya mwanamke huyo na mwanaye, Frank Hilari, ambapo mama huyo alitoka mbio na kukimbilia nyumba ya jirani.
Hata hivyo mashuhuda hao ambao walikataa majina yao kutajwa, walidai baada ya hali hiyo, mtoto huyo,  alimfuata nyuma mama yake na kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa na mwanamke mmoja mzee, ambaye alishindwa kuamulia na kumpiga shoka mama yake, na kusababisha kifo chake.

No comments:

Post a Comment