Pages

Monday, March 18, 2013

Mtawa apigwa risasi, aporwa Sh20 mil



Arusha. Watu wanaoaminika kuwa ni majambazi, wamemjeruhi kwa kumpiga risasi Mtawa wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha, Shobana Synd na kumpora kiasi kikubwa cha fedha.
Habari kutoka kwa wenzake zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas zinasema kuwa mtawa huyo raia wa India kutoka Shirika la Notre Dame, alishambuliwa kabla ya kuporwa fedha hizo.
Kwa mujibu habari hizo, mtawa huyo aliyekuwa akitoka benki, alijeruhiwa kwa risasi mbili wakati akisubiri kufunguliwa geti la kuingia katika Shule ya Msingi Notre Dame.
Ingawa Watawa hao hawakuwa tayari kutaja kiasi cha fedha zilizoporwa, habari zinasema ni zaidi ya Sh20 milioni zilizochukuliwa benki kwa ajili ya malipo na shughuli mbalimbali za shule hiyo.

No comments:

Post a Comment