Pages

Tuesday, March 12, 2013

Watatu wapoteza maisha mkoani Singida katika ajali ya basi kutokana na uzembe wa dereva na mwendo kasi.



Abiria mmoja raia wa nchini China, ambaye jina lake halikufahamika mara moja ambaye amevunjika mguu wa kushoto akipewa huduma za matibabu mara baada ya ajali ya basi la Green star lililogonga lori la mbao katika eneo la kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi.
Baadhi ya majeruhi wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa wa Singida,wakisubiri kupata matibabu.
Baadhi ya wakazi wa mji wa Singida,wakiwa nje ya maabara ya hospitali ya mkoa,kuwaona majeruhi wa ajali ya basi la Green star iliyotokea jana (10/3/2013) katika kijiji cha Isuna wilaya ya Ikungi.(Picha na Nathaniel Limu).
Watu watatu wamefariki dunia baada ya basi T.939 BRA aina ya Yutong, lililokuwa likitokea Dar-es-salaam likielekea Kahama mkoani Shinyanga, kugonga kwa nyuma lori T.268 CCC  likivuta tela T.931 CBU aina ya Scania.

No comments:

Post a Comment