Pages

Thursday, April 25, 2013

AIBU SANA : MTOTO WA KIGOGO ABABWA KATIKA OPERATION YA UKAHABA , BIBI HARUSI AFUMANIWA AKIFANYA NGONO KWENYWE BAJAJI



Katika oparesheni hiyo iliyofanyika usiku wa Jumapili iliyopita watu kibao walinaswa hasa katika Ufukwe wa Coco, jijini Dar akiwemo bibi harusi mmoja na mtoto wa kigogo




BIBI HARUSI LAIVU KWENYE BAJAJ

Kwenye ufukwe huo, mwanamke mmoja ambaye jina halikupatikana, aliyedaiwa kufunga ndoa Ijumaa iliyopita, naye alikamatwa katika msako baada ya kunaswa na mwanaume wakifanya ngono kwenye Bajaj.
Katika tukio hilo, mwanaume alifanikiwa kutoka nduki huku akimwacha demu wake akijikusanya kwa kuvaa nguo.
Mwanamke huyo naye alifanikiwa kuwatoka askari hao na kukimbilia chooni ambapo aliwakuta wanawake wengine waliojificha hivyo wakakamatwa wote kwa pamoja.
Ili kuweka ushahidi, askari hao wa kazi waliikamata Bajaj hiyo.

ALIKWENDA KUKUMBUSHIA ENZI ZAKE

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, mkazi wa Kinondoni-Manyanya, usiku huo alifika mahali hapo kukumbushia enzi zake kabla ya kuolewa ambapo ilidaiwa kwamba alikuwa akijiuza ufukweni hapo.
Alijitetea kuwa mume wake alisafiri hivyo akaona akakumbushie enzi zake kabla hata ‘hina’ aliyopakwa wakati wa harusi haijafutika mwilini.
Pamoja na maelezo hayo, mwanamke huyo aliishia kwenye ‘difenda’ la polisi tayari kwa kupelekwa kituoni kwa maelezo zaidi.

BINTI WA KIGOGO
Katika kundi hilo la wanawake na wanaume zaidi ya hamsini waliokamatwa ufukweni hapo usiku huo wa saa 9 na ushee, kulikuwa na mtoto wa kigogo mmoja serikalini katika idara nyeti ambaye alinaswa mchangani baharini akiwa kwenye kundi la makahaba.
Mtoto huyo aligundulika kuwa ni binti wa mnene wakati wa kutoa maelezo kituoni Oysterbay.

MASIKINI ALIKUWA NA ‘BOIFRENDI’ WAKE

Akijitetea wakati wa kutoa maelezo, binti huyo aliyeonekana mrembo na mwenye mvuto wa ajabu, alisema kwamba alikuwa na ‘boifrendi’ wake na kuwa alitoroka kwao usiku huo.
Binti huyo aliomba chondechonde asipigwe picha kwani endapo itaonekana gazetini basi atakuwa amejipalia makaa nyumbani kwa vile hataeleweka kwa sababu anapatiwa fedha za matumizi pamoja na ada ya shule.
Ukiacha mwanamke na binti huyo wa kigogo, wanawake wengine wengi walikamatwa, wengi wao walikutwa wakifanya vitendo vya ngono mchangani wakiwa ‘pea’.
MACHANGU WAFUNGUKA
Kati ya wote waliokamatwa, wanawake kumi na tano walikiri kujishughulisha na biashara ya kuuza miili ambapo walisema wanafanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.

ACD MUTAFUNGWA ANASEMAJE?

Kwa upande wake OCD Mutafungwa alisema wameamua kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi kwa kuvamia eneo hilo.


INSPEKTA SWAI ATIA NENO
Naye Inspekta Swai aliyekuwa ‘front’ katika zoezi hilo alisema kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu kila wiki ili kukomesha vitendo viovu katika ufukwe huo.
NI MATOKEO YA GAZETI LA RISASI
Oparesheni hiyo ilikuja siku chache baada ya gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 1000 la Jumatano ya Aprili 17-19 kuripoti ufuska unaofanyika katika ufukwe huo usiku wa saa 9 na kuendelea.  
Uchunguzi wa gazeti hilo ulieleza kiundani vitendo vya ngono, usagaji, ubakaji, ushoga na ujambazi vilivyokuwa vikifanyika eneo hilo hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni wakaona kuna kila sababu ya kufumua uozo huo kwa kuwa ni wachapakazi.


source Gazet La RISASI

No comments:

Post a Comment