Simoni Lazaro (kushoto) akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Gerald Mango.
Charles Kijuba akikwepa kamera mahakamani.
MAOFISA
watatu waandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi leo
wameburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za
ufujaji wa pesa za serikali zaidi ya milioni 200. Watuhumiwa hao ni
Simon Lazaro ambaye alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera,
Gerald Mango, Mkuu wa Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi , na Charles
Kijuba, Kaimu Mhasibu Mkuu.Watuhumiwa hao wamekana mashitaka na mahakama hiyo imesema kuwa dhamana iko wazi
No comments:
Post a Comment