Pages

Thursday, April 18, 2013

HUKUMU YA PONDA YAINGIA DOSARI



Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Sheikhe Ponda Issa Ponda akihutubia baadhi ya wafuasi wake.
 
HUKUMU ya Kesi inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya maandamano haramu imeahirishwa mpaka tarehe 9 mei mwaka huu.

Kesi hiyo imeharishwa baada ya Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa ,kutokuwepo Mahakamani hapo.

Awali hakimu huyo alitarajiwa kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu ya kesi hiyo Na.245/2012 inayomkabili Ponda na wenzake. 

Aprili 3 mwaka huu:Mawakili wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment