Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, April 13, 2013

MKAGUZI ATAKA M-PESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY, EASY PESA ZITOZWE KODI...



Ludovick Utouh.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ameshauri kampuni za simu zinazotoa huduma ya utumaji fedha na kumbi za harusi vitozwe kodi.


Sambamba na hilo aliutaka uongozi wa Bunge, kurejesha Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).
Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasilisha taarifa yake bungeni mjini hapa jana akisema uamuzi wa kufuta kamati hiyo na kazi zake kuunganishwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), hautakidhi matarajio ya wadau wa uwajibikaji.
Kwa upande wa kodi, alishauri kodi kutoka kwa wafanyabiashara wadogo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ihusishe kikamilifu makatibu kata kutambua walipa kodi wakiwamo wamiliki wa kumbi za harusi na mikutano.

No comments:

Post a Comment