Pages

Thursday, April 25, 2013

MVUA YAVUNJA PAMBANO LA LIGI YA TAIFA MANISPAA YA MORO.



 Mchezaji wa Compassion[no 3] akijaribu kumiliki mpira kwenye dimbwi la maji jioni hii 
MCHEZO wa ligi ya taifa daraja la nne manispaa ya Morogoro kati ya timu ya Terminal inayomilikiwa na wapiga debe wa stendi ya mabasi ya Msamvu na timu ya Compassion inayomilikiwa na kanisa la Aglikana umevunjika dakaika ya 20 baada ya mvua kubwa kunyesha muda mfupia baada ya mchezo huo kuanza.Hali hiyo ilisababsiha uwanja wa saba saba kujaa maji na kusababsiha wachezaji kushindwa kumuiliki mpira huku wachezaji hao wakianguka hovyo.Mvua hiyo ambayo mapaka sasa inaendela kunyesha ilisababisha uwanja huo kujaa maji hivyo mwamuzi wa mchezo huo aliyefahjamika kwa jina moja la Simba baada ya kujadiliana na uongozi wa kamati ya ligi hiyo alimu kuvunja mchezo huo dakika ya 20.Kaimu mwenyekiti wa chama cha soka manispaa ya Morogoro Boniface Kiwale alipotakiwa kuelezea hatima ya mchezo huo alidai kwamba utaludiwa siku nyingine.
                  mchezo huo ukiendelea kwenye madimbwi ya maji
Hadi mchezo huo unavunjika timu hizo zilikuwa hazijafungana huku Terminal wanaongoza ligi hiyo walioneka kumilika mpira kwa dakika zote 20.Ligi hiyo itaendela kesho kwa Mawenzi market inayomilikiwa na wafanyabiashra wa soko la matunda la Mawezi ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo watakipiga na Sultan Area inayosbuluza mkia kwenye ligi hiyo

 Baada ya mvua hiyo inayoendelea kunyesha kwa sasa mwamuzi wa mchezo huo aliyefahamika kwa jina  moja la Simba akitoka uwanjana na kwenda kujadiliana na makati ya ligi hiyo kufuatia uwanja huo wa saba saba kujaa maji

                        Wachezaji wakisubili wakati wajadiliano hayo yakiendelea
Baada ya kujadiliana na uongozi wa kamati ya ligi hiyo mwamuzi Simba,aliamu kuvunja pambano hilo baada ya uwanja kujaa maji,picha mwamuzi huyo akichukua mpira kwa lengo la kuvunja mchezo huo.

No comments:

Post a Comment