Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika
mazungumzo Rasmi na ujumbe wa Serikali ya Uholanzi ukiongozwa na Waziri
wa Mambo ya nchi za nje wan chi hiyo Bwana Frans Timmermans jijini The
Hague Uholanzi.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi
hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi. Waziri
wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi
hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi. Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha mbegu bora za mazao ya mboga ya Rijk
Zwaan Bwana Kees Reinink akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
baadhi ya miche inayotokana na mbegu bora wakati Rais alipotembelea
makao makuu ya Kampuni hiyo katika kitongoji cha De Lier nje kidogo ya
jiji la The Hague,nchini Uholanzi jana. Wapili kushoto ni Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SAGCOT Bwana
Geoffrey Kirenga.Kampuni ya RIJK ZWAAN tayari imewekeza nchini Tanzania
huko Arusha ambapo inazalisha mbegu bora za mazo ya mbogamboga
zilizofanyiwa utafiti kudhibiti magonjwa. Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Utafiti
na Uzalishaji mbegu bora za mazao ya mboga ya RIJK ZWAAN jana katika
kitongoji cha De Lier nje kidogo ya jiji la The Hague.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa pamoja na
Malkia Beatrix wa Uholanzi wakati walipomtembelea Malkia huyo katika
makazi yake Rasmi jijini The Hague jana.Rais Kikwete yupo nchi Uholanzi
kwa Ziara rasmi.Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment