Pages

Thursday, April 18, 2013

TIMU YA FAR RABAT YAWASILI DAR KUIKABILI AZAM FC JUMAMOSi



Wachezaji wa timu ya Far Rabat, wakiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo tayari kuwakabili wapinzani wao, Azam Fc katika mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya pili, unaotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, jumamosi ya wiki hii.

AKIZUNGUMZA  na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Nahodha wa timu ya Far Rabat Bellakhdar Younes, amesema kuwa  timu yake ipo kamili na inauhakika wa kuifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika utakaochezwa uwanja wa Taifa jumamosi wiki hii.

“Timu yetu ni nzuri na Azam pia ni wazuri kwani wana wachezaji waliopo kwenye timu ya taifa hivyo tutahakikisha tunafunga mabao 2-0 ili iwe rahisi wakija nyumbani”, alisema Younes.

Wachezaji wa Far Rabat ambao wapo kwenye timu ya Taifa ya Morocco ni Hammal Younes, Achchakir Abderrahim, Bellakhdar Younes, Saidi Salaheddine, Aqqal Salaheddine na Youssef Kaddior.

Timu hiyo imewasili ikiwa na msafara  wa watu 31 na umefikia kwenye hoteli ya Saphire iliyoko Kariakoo.

Baadhi ya viongozi wa timu hiyo wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili jana mchana. Picha na Lenzi ya Michezo.

No comments:

Post a Comment