Na Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewapa
siku 10 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulipa deni la Sh. 573, 525,
673.8 kuanzia Jumatatu au wakate Rufaa.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka TRA, Maofisa
wa Mamlaka hayo walifanya tathmini Machi 14, mwaka huu kutokana na
ukaguzi wa hesabu za shirikisho hilo na kukuta wana deni linalotokana na
kodi za Lipa Kadiri Unavyoingiza (PAYE) na Ongezeko la Thamani (VAT) la
jumla ya Sh. 573, 525,673.8.
Kufuatia hali hiyo, TRA ikawaandikia barua TFF ikiwataka walipe ndani ya siku 10 kuanzia Jumatatu au wakate Rufaa.
No comments:
Post a Comment