WANAWAKE
wawili katika Manispaa ya Musoma maeneo tofauti wamejinyonga huku
mmoja akijinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na mwingine akijinyonga
kwa kutumia mtandio wa nguo yake
Katika
tukio la kwanza mwanamke aitwaye Rudia kyango umri wa miaka 40 Mkazi
wa kata ya Kigera Manispaa ya Musoma amekutwa amekufa kufuatia
kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na kuleta simanzi kubwa kwa
familia yake.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia april 13 mwaka huu ambapo marehemu
alijinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali na kufariki dunia na mara
baada ya wakazi wa eneo hilo kufika nyumbani kwa marehemu walitoa
taarifa katika kituo kidogo cha polisi kigera na polisi kuuchukua
mwili wa marehemu kwa kwaajili ya uchunguzi wa kitabibu katika
hospitali ya mkoa wa mara.
Wakati
huo huo Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Bhoke au mama
marwa Mkazi wa Mtaa wa Ghandhi manispaa ya musoma anayekadiliwa kuwa
na umri wa miaka 27 hadi 30 amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia mtandio
wa nguo yake akiwa chumbani.
Tukio
hilo limetokea asubuhi leo (jana) katika mtaa wa ghandi mjini Musoma
baada ya watoto wake kwenda shuleni ambapo majirani walimshuhudia na
kutoa taarifa polisi.
Majirani
hao waliiambia blog hii Mwanamke huyo huenda alichukua maamuzi hayo
baada ya watoto wake kwenda shuleni na kubaki pekee yake nyumbani.
wamekumbana na mama huyo akiwa amejipiga kitanzi shingoni kwa kutumia mtandio wa nguo na kufariki dunia.
Umati
wa wakazi wa Manispaa ya Musoma ulijaa katika eneo la tukio huku
simanzi zikitawala kufuatia kifo hicho cha kujinyonga ambapo marehemu
kabla ya kifo chake alikuwa anafanya kazi kwa mtu binafsi ya kuuza
vinywaji baridi.
Jeshi
la polisi lilifika katika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu
kwaajili ya uchunguzi wa kitabibu na pia kuchunguza kubaini
kilichopelekea kifo cha marehemu huyo.
Source: Shomm Binda
No comments:
Post a Comment