Pages

Wednesday, April 24, 2013

UWOYA KUJIPATI MILIONI 200 ZA BUREEEEE KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS. SOMA MCHEZO WOTE HAPA


DIVA anayetesa katika sinema za Bongo, Irene Pancras Uwoya ananukia utajiri ambapo hivi karibuni ‘anatarajia’ kuogelea kwenye
 
Mfano wa sehemu ya fedha atazolipwa Uwoya
mamilioni ya fedha kwa kukomba Shilingi Milioni 200 za madafu, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu mkobani.
Uwoya ni mke halali wa msakata kabumbu wa kulipwa nchini Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ambapo ndoa yao ilifungwa
mwaka 2009 katika Kanisa Katoloki, Parokia ya Mt. Joseph, Posta jijini Dar es Salaam.

KUTOKA DAR ES SALAAM
Msanii huyo ambaye hakaukwi na skendo, huenda akaibuka milionea ikithibitika kwamba habari iliyoandikwa na gazeti damu moja

na hili, Ijumaa Wikienda la Jumatatu Aprili 8 – 14, toleo namba 310 iliyokuwa na kichwa; UWOYA, DIAMOND WANASWA

HOTELINI ni ya uongo.
Habari kutoka katika vyanzo vyetu vya kuaminika, zinasema kuwa  mdada huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwaye Krish

Hamad Ndikumana yu mbioni kuandika barua ya madai kupitia kwa mawakili wake  waliopo Dar ili kudai fedha hizo kwa maelezo

(eti) alichafuliwa na kuingiliwa faragha yake.

KIVIPI SASA?
Moja ya vyanzo hivyo ambacho ni shosti wa karibu na Uwoya alilieleza gazeti hili kuwa baada ya habari ile kutoka gazetini,

mawakili hao walimfuata na kumwambia kuwa pamoja na machungu aliyoyapata, habari ile kwake ni dili na inaweza kubadili

maisha yake (mh!).
“Amefuatwa na mawakili zaidi ya wanne kwa nyakati tofauti lakini kuna mmoja anaonekana kumuamini zaidi ndiye anayedili naye

kwa sasa. Huyo wakili amemhakikishia kuchukua hizo fedha kwa kuwa zipo njenje,” alisema shosti huyo na kuongeza:
“Kikubwa alichomwambia huyo wakili ni kwamba ile habari imemdhalilisha na imeingilia uhuru wa faragha yake kinyume na sheria

ya nchi yetu.”
Akaongeza: “Amemhakikishia kutumia ufundi wake wote kuandika barua yenye vitisho vitakavyosaidia kulifanya gazeti hilo litoe

hizo fedha kabla ya suala hilo kufikishwa mahakamani kupambana kwenye sheria.” (tuko ngangari).

NI FARAGHA IPI HIYO?
Chanzo hicho kimeendelea kufafanua kuwa wakili wa Uwoya amemweleza kwamba barua yake hiyo ya madai itaandikwa kwa

kuzingatia mwongozo wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kwa maelezo yake imevunjwa.
Habari za moto zinapasha kuwa, barua hiyo itazingatia kuvunjwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 16

kifungu kidogo cha 1 ambacho kimekataza watu kuingiliwa katika faragha zao.
“Kiukweli ana imani naye sana na amemhakikishia kuzoa hizo fedha kwa sababu ana ufahamu mkubwa na sheria na namna ya

kupanga maneno katika barua hiyo,” alisema.

KUKUNUA GARI, KUJENGA NYUMBA YA KIFAHARI
Pekupeku za Risasi Mchanganyiko zinaeleza kwamba kwa sasa Uwoya ana uhakika wa kubadilisha maisha yake mara baada ya

utaratibu wa barua hiyo kukamilika na kufika kwa uongozi wa Global Publishers.
Imeelezwa kwamba, kitu cha kwanza ambacho Uwoya amepanga kufanya ni kununua gari la kifahari na kuachana na analotumia

sasa ambalo si lake huku mpango wa pili ukiwa ni kujenga nyumba bora ya kisasa. (Uwoya bwana!)
“Anataka kuanza kuishi maisha ya kistaa zaidi, anasema eti gari analotumia sasa hivi halifanani na hadhi yake. Kitu kingine

anachofikiria ni kujenga nyumba ya kifahari Mbezi Beach (kwenye upepo mwanana). Anasema kule ni pazuri zaidi kwa sababu ni

nyumbani kwao.
“Hivi ninavyozungumza na wewe tayari ameshaonana  na wataalam wa ramani ili waweze kumshauri mjengo mzuri wa kisasa

ambao ataujenga baada ya kuchukua hizo fedha,” alisema.

MHARIRI KIZIMBANI
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda lililotoa habari hiyo ya Uwoya na Diamond kunaswa (jina kapuni) alipatikana juzi Jumatatu

jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka yake ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha.
Akizungumza kwa kujiamini, mhariri huyo alisema: “Bado sijapokea barua ya namna hiyo lakini ikija itanishangaza sana. Kufupi

nipo tayari kupambana na hiyo kesi kwa sababu waandishi wangu walifanya kazi nzuri na upo ushahidi wa kutosha mezani kwangu,

 waje tu. Teeh! Teeeh! Teeeeeh!”
Kuhusu gazeti lake kuingilia faragha ya Uwoya kama madai yanavyoeleza, mhariri: “Ni faragha ipi hiyo iliyoingiliwa kwa Uwoya na

Diamond? Ukisoma ile habari mstari kwa mstari na kutazama zile picha, utaona kwamba kilichoripotiwa ni wao kunaswa hotelini

wakiingia usiku na kutoka siku inayofuata.
“Hakuna picha wala aya yoyote katika ile habari iliyoonesha kwamba, waandishi wangu walimfuata Uwoya na Diamond chumbani

walipokuwa kwenye faragha yao. Labda walipokuwa mapokezi na kupita kwenye korido ndiyo faragha yao! Ha! Haa! Haaa!
“Tuliripoti  kunaswa hotelini tu hasa kwa kuwa tunajua kuwa Uwoya ni mke wa mtu na Diamond ana mchumba. Ni hivyo tu.

Hakuna cha kujadili sana hapa ndugu mwandishi teh!”

HEBU PATA PICHA KIDOGO
Katika habari inayodaiwa kulalamikiwa na Uwoya hadi kufikia kukubaliana na wakili wake kupeleka barua ya madai, ilieleza hatua

kwa hatua ya namna mastaa hao  walivyoingia katika hoteli moja ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano (jina lipo), Mbezi Beach

jijini Dar es Salaam na kuishia katika chumba namba 208.
Upo ushahidi wa picha za mnato na video zikimwonesha Diamond ambaye muda mfupi baada ya kuingia katika chumba hicho

alitoka mapokezi kulipa na kuandikisha akiwa amevaa viatu vya Uwoya (video ipo jamani).
Baada ya kuingia katika chumba namba 208 alichokuwa Uwoya mishale ya saa 8:24 usiku, wote wawili hawakutoka hadi kesho

yake, saa 9:00 mchana.
Awali, wakati wanaingia katika hoteli hiyo ambayo tayari ilikuwa chini ya ulinzi wa mapaparazi wa Global, Diamond alikuwa na gari

la Uwoya aina ya Toyota Fortuner na Uwoya alikuwa na la Diamond, Toyota Land Cruiser Prado (picha kibao zipo zikionesha

hivyo).
Baada ya mkesha wao, wakati wa kuondoka kila mmoja aliondoka kivyake kwa kutumia gari lake.

KICHEKESHO CHA UWOYA
Mara baada ya habari hiyo inayodaiwa kupangiwa kuzolea mamilioni ya shilingi kutoka kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Uwoya

alipiga simu kwa waandishi mbalimbali wa Global na kulalamika  kwamba habari ile inaweza kuharibu ndoa yake.
Uwoya, huku akijua muda mrefu kwamba kuna tetesi za yeye kutoka na Diamond, alimpigia simu mmoja wa waandishi wetu na

kusema: “Yametimia. Sijui kama kuna ndoa tena. Kila kitu kimeharibika sasa, lakini kwa nini hamkunipa nafasi ya kuzungumza

kwanza?”
Hata hivyo, alipopata nafasi ya kuzungumza na paparazi mwingine, Uwoya hakuwa na cha maana cha kujieleza zaidi ya

kujibaraguza na kudai kuwa habari ile imemfedhehesha na kwamba hawezi kutoka kimapenzi na Diamond.
Uwoya alipoelezwa kwamba timu ilikuwa na ushahidi wa kutosha wa picha za video alikanusha na kudai kuwa angeweza kuja

kuziona ofisini ili kujiridhisha. Hata hivyo, hakutokea mpaka giza linaingia siku hiyo.
Kwa upande mwingine, Uwoya alimwambia mwandishi mwingine: “Ndoa yangu imevunjika rasmi asubuhi hii. Mume wangu

alizimia baada ya kuiona ile habari yenu, nyienyie.” (mazungumzo hayo yemerekodiwa, siku akitaka afike Global na mawakili wake

wasikie sauti).

WADAU WAKE JE?
Kabla ya mchana wa siku ambayo habari hiyo ilitoka, tayari stori hiyo ilikuwa imeshasambaa katika mitandao mbalimbali ya

kijamii na wadau walitoa maoni yao, wengi wakimshambulia Uwoya kwa kuacha ndoa yake na kwenda kujirusha na ‘bwana mdogo’

sana, Diamond.
“Mtoa maoni mmoja alitupia hivi: “Mh! Bado sijapata picha ya sampuli ya Uwoya. Ni mwanamke wa aina gani? Si juzi tu alipatana

na mumewe sasa inakuwaje anakutwa na Diamond usiku hotelini?”

IRENE UWOYA NI NANI?
Irene Uwoya ni Miss Tanzania namba 5, mwaka 2006 akitanguliwa na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Lissa Jensen na Victoria

Martin. Kwenye filamu aliibuliwa na Lucy Komba katika katika sinema yake iliyomkutanisha na Yusuf Mlela.
Kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa Bongo Movie Unit akiwa chini ya Mwenyekiti Vincent Kigosi ‘Ray’.

KIFUATACHO
Baada ya kumheshimu na kutunza siri zake kwa muda wote huo, Global Publishers imejipanga kuvunja ukimya kwa kuanika video

ya Uwoya na Diamond hatua kwa hatua kuanzia walipoingia hotelini.
Zoezi hilo litafanyika mapema sana mara baada ya kujiridhisha kwamba ni kweli anatarajia au amefikisha barua hiyo ya madai

katika ofisi  za Global.
Mtandao namba moja kwa burudani Bongo, www.globalpublisherstz.com ndiyo utakuwa wa kwanza kuanika kabla ya kuhamishia

kwenye mitandao mingine ya kijamii ukiwemo ule maarufu wa Youtube ili kutoa nafasi kwa Watanzania kuona kama ‘Oparesheni

Fichua Maovu ya Global’ inafanya kazi kweli au ni fiksi tu na faragha iliyoingiliwa ni ipi?!
CHANZO : GPL

1 comment:

  1. uwoya ni sawa na dekio la chooni!!!!!!hata wanaume wanaompapatikia hazijatimia kichwani ,,ni hayo tu

    ReplyDelete