Matukio kama haya ya watu kujichukulia sheria mikononi na kuwauwa wenzao kwa kuwachoma moto yamekithiri katika jamii na ndiyo yaliyosababisha ajuza watatu kuuwawa kikatili usiku wa kuamkia leo huko Bunda, Mara |
MAUAJI
ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara
baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja
kama Kuku kisha kuwachoma moto ajuza watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha
na vitendo vya kishirikina.
Pia watu
hao mbali na kuwaua kikatili vibibi hivyo kwa tuhuma kwamba walimuua
kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba
walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga
na kuatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa mujibu
wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio
hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira
kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua
kijana huyo hivi karibuni.
Inaelezwa
kijana huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga
alidai hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa tangu
azikwe kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za
usiku pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo
wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo.
Inaelezwa
ndipo walipotajiwa majina ya wanavijiji watatu wa kijiji hicho ambao
hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja na familia zao
kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na kuangushiwa adhabu hizo
za kinyama.
Wa kwanza
kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye alikimbilia kijiji
cha jiorani kwa rafikie aitwaye Bi Laya, ambapo walimtaka miguu yote
miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla ya kumchoma moto
ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua nguo zake tu huku
mwili ukiwa upo vile vile.
Baadaye
walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama
kama rafikie kwa kile walichodai kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa
kuamini huenda wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye
kurudi Kasaula na kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia
ajuza hao wengine kisha kuchoma nyumba tatu.
Bibi wa
tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo, lakini
nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga kuporwa na
watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo kuwachoma na
kuwala kwa hasira.
Kamanda wa Polisi wa Bunda, Mika David
Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo la kusikitisha na kwamba
wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka waliohusika na kitendo hicho
cha kujichukulia sheria mikononi.
No comments:
Post a Comment